img

Mazungumzo kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya “bado ni magumu”

December 13, 2020

 

Mazungumzo kuhusu mkataba wa kibiashara kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit yameendelea usiku wa kuamkia leo mjini Brussels lakini duru zinasema “yamesalia kuwa magumu”Maafisa kadhaa walio karibu na ujumbe wa Uingereza kwenye mazungumzo hayo wamedokeza kwamba huenda majadiliano zaidi yataendelea leo kwa imani yanaweza kufanikisha kupatikana mkataba.

Kadhalika waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepangiwa baadae leo kuwa na mazungumzo mengine na rais wa Halmshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen kuhusu hatma ya majadiliano yanayoendelea.

Leo Jumapili ndiyo muda wa mwisho kwa kila upande kuamua iwapo mazungumzo hayo yanaweza kuendelea au Uingereza iondoke kutoka Umoja wa Ulaya bila ya kuwa na mkataba.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *