img

Marekani kuanza kutoa chanjo ya COVID-19 siku ya Jumatatu

December 13, 2020

 

Maafisa wa Marekani wamesema chanjo ya virusi vya corana iliyotengenezwa na kampuni mbili za Pfizer na BioNTech itaanza kutolewa kwa mara ya kwanza kesho Jumatatu siku kadhaa tangu matumizi yake yalipoidhinishwa.

Jenerali wa Jeshi la Marekani anayesimamia usambazaji wa chanjo hiyo, Gus Perna, amesema dozi za kwanza zitasafirishwa leo Jumapili na hapo kesho zoezi ya utoaji chanjo litaanza kwa asilimia 100.

Perna amearifu kuwa ifikapo kesho vituo vya kutolea chanjo 145 vitakuwa vimepokea shehena ya kwanza, huku vituo 425 vitapelekewa chanjo siku ya Jumanne na chanjo hiyo itapokelewa pia kwenye vituo vingine 66 siku ya Jumatano.

Katika awamu hiyo ya kwanza watu milioni 3 watapatiwa chanjo huku watumishi wa afya na wahudumu walio mstari wa mbele watapewa kipaumbele katika utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *