img

Kanuni za kunyunyizia dawa shambani

December 13, 2020

 

Nakukalibisha mpenzi msomaji wa blog yetu pendwa, nahuu niwakati mwingine tena wa kuendelea kujifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na kilimo. Na leo nitakuelezea kanuni za kunyunyuzia dawa shambani.

Awali ya yote nataka kukuelezea maana ya kunyunyuzia dawa au spraying kwa lugha ya kitaalamu. kunyunyuzia(spraying) nikitendo cha kulinda mazao na wadudu na magonjwa kwa kusambaza kiasi kidogo cha viwatilifu katika mmea mama.

 Kemikali unyunyuziwa kama mchanganyiko kwa kiasi kidogo, kati au kikubwa juu ya mmea mama ili kuulinda na wadudu au ugonjwa flani kwa hali ya kimiminika.

Vifaa tofauti tofauti vya kunyunyuzia dawa/ viwatilifu
Aina tofauti tofauti ya vinyunyuzi hutumiwa kulingana na aina ya zao, kipato cha mkulimwa na ukubwa wa shamba, vifuatavyo ni vifaa hivyo.

AERIAL SPRAYER; hiki ni kifaa kinacho huusisha ndege katika kunyunyuzia, ni mahususi katika zao la viazi au mazao mengine ya mboga mboga ambayo uhitaji kutibiwa katika kipindi ambacho mataili ya trekta yanaweza kujeruhi mazao hayo.

MANUAL KNAPSACK SPRAYER; Hiki ni kifaa ambacho mnyunyuziaji hukibeba mgongoni na kutumia mkono wake mmoja kupamp na mwingine kuelekeza nozzle katika mazao, na kifaa hiki hubeba little 5 hadi 15 za dawa iliyo changanya na maji.

MOTORIZED KNAPSACK SPRAYER; Hiki ni kifaa ambacho pia kinafanana na nilicho kitaja mara ya pili, tofauti yake hiki kinakua na engine ambayo huzunguka na kuwezesha dawa kwenda umbali mrefu, kifaa hiki utumiwa mahali ambapo Manual knapsack sprayer kinakua hakina uwezo wa kufikisha mfano miti. na kifaa hiku hubeba little 15 hadi 20.

TREE SPRAYER; Hiki kifaa hutumika kunyunyuzia dawa katika miti midogo, mfano miti ya matunda.

BOOM SPRAYER; Pia kifaa hiki hutumika kunyunyuzia dawa katika mashamba makubwa sana, na hufanya kazi kwa kuambatanisha katika trekta. kifaa hiki ubeba litter tofauti tofauti mfano 4000, 6000 nakadhalika.

Kanuni za kunyunyuzia dawa.
Zifuatazo ni kanunu muhimu ambazo unatakiwa uzingatie wakati wa kunyunyuzia dawa.
angalia uelekeo wa upepo kabla ya kunyunyuzia dawa,
Nilazima uvae vifaa vya kukulinda mfano groves na mask
Hakikisha kifaa chako kimefungwa vizuri
Osha kifaa chako cha kunyunyuzia kabla na baada ya kukitumia
Tunza kifaa chako mahali safi na kavu
Changanya na koroga dawa yako vizuri kabla ya kunyunyuzia
Hakikisha unatumia vipo sahihi.

Bila shaka mpenzi msomaji umejifunza mengi zaidi katika somo hili.
,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *