img

Kansela Merkel kujadili hatua kali kudhibiti virusi vya corona

December 13, 2020

 

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anatarajiwa leo kukutana na viongozi wakuu wa majimbo 16 kujadili hatua ziada za kukabiliana na ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona.

Majadiliano ya leo yatafanyika wakati maafisa wa ngazi ya juu nchini Ujerumani wanatoa wito wa kutangazwa marufuku kali zaidi kudhibiti kuenea virusi vya corona pamoja na rikodi ya juu ya maambukizi inayotia wasiwasi.

Taasisi ya kudhibiti magonjwa nchini Ujerumani ya Robert Koch ilirekodi visa vipya 28,438 katika muda saa 24 zilizopita pamoja na vifo 496 kutokana na COVID-19 idadi ambayo ni kubwa kuwahi kushudiwa nchini humu.

Ujerumani ambayo wakati wa msimu wa machipuko ilikuwa na kiwango kidogo cha vifo ikilinganishwa na mataifa mengine jirani hivi sasa imefikisha idadi ya vifo 21,466 pamoja na maambukizi milioni 1.3 ya virusi vya corona.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *