img

Iran yamuita balozi wa Ujerumani kumhoji juu ya ukosoaji uliotoka Umoja wa Ulaya

December 13, 2020

 

Iran imemuita kwa lengo la kumuhoji balozi wa Ujerumani ambayo inashikilia kwa sasa uongozi wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya,kuhusu ukosoaji unaotolewa na Umoja huo kufuatia kuuwawa kwa mwandishi habari wakiiran. 

Vyombo vya habari vya Iran vimetangaza leo kwamba wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo pia inapanga leo Jumapili kumuhoji balozi wa Ufaransa mjini Tehran. 

Ufaransa ni miongoni mwa nchi zilizokosoa vikali hukumu ya kuuwawa jana jumamosi mwandishi habari mkosoaji wa serikali ya Iran, Ruhollah Zam ambaye makao yake yalikuwa Paris kabla ya kukamatwa kwake na kupelekwa Iran. 

Zam alishtakiwa kwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya Iran mwaka 2017. Mtandao wake wa habari wa AmadNews ulifuatiliwa na watu milioni 1.

Baada ya hukumu ya kuuliwa kwake kutekelezwa Umoja wa Ulaya ulitowa taarifa ukilaani hatua hiyo kwa maneno makali na kuipinga vikali kwa mara nyingine adhabu hiyo ya kifo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *