img

Uingereza kusitisha ufadhili kwa sekta ya usafirishaji mafuta ya petroli na gesi asili

December 12, 2020

Uingereza imetangaza jana Ijumaa kwamba inasitisha ufadhili kwa sekta ya usafirishaji mafuta ya petroli na kuelekeza uungaji mkono kwa miradi ya nishati salama na yenye kuzalisha kiwango kidogo cha gesi ukaa.

Tangazo hilo lililotolewa na waziri mkuu Boris Johnson limekuja wakati Uingereza itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele unaofanyika leo kuadhimisha miaka mitano ya mkataba wa kihistoria wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Johnson amesema kupitia uamuzi huo aloutaja kuwa madhubiti Uingereza itatengezena nafasi nyingi za ajira, kufufua uchumi baada ya janga la virusi vya corana na kuilinda sayari ya dunia kwa manufaa ya vizazi vinavyokuja.

Chini ya hatua hiyo serikali mjini London, itasitisha msaada wa kifedha kwa usafirishaji nje bidhaa za mafuta ya petroli pamoja na ruzuku kwa miradi mipya ya mafuta, gesi asili na uzalioshaji nishati kwa kutumia makaa ya mawe.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *