img

TAKUKURU yawafunda wahitimu wa shule ya sekondari Mnero

December 12, 2020

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Tamaa, anasa, sitarehe na kupenda mafanikio ya haraka ya maisha kwa njia za mkato vimetajwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayo changia baadhi ya vijana kujiingiza kwenye magenge ya uhalifu.

Hayo yalielezwa jana na mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)  wa wilaya ya Nachingwea, Budi Ebrahim wakati wa mahafali ya 27 ya shule ya sekondari ya Mnero iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.

Akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne kwenye mahafali hayo, Budi alisema miongoni mwa sababu zinazosababisha vijana wengi kujiingiza na kufanya vitendo vya uhalifu ni tamaa, starehe na kutaka mafanikio ya haraka kwa njia za mkato. Huku wakikwepa kufanya kazi halali kwa juhudi na maarifa.

Alisema vijana wengi wana tamaa na wanataka starehe na anasa wakati hawapendi kufanya kazi halali zinazotokana na fursa zinazo wazunguka. Kwahiyo wanaamua kujiingiza kwenye magenge ya uhalifu ili kutimiza ndoto zao kirahisi.

Aliwaasa wahitimu hao kwamba hata ambao hawatabahatika kuchaguliwa kuendelea na elimu ya juu wanayo nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zao za maendeleo iwapo watatumia fursa zinazo wazunguka kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa bila kuvunja sheria za nchi.

Alionya kwamba anasa na starehe ni miongoni mwa mambo yasiyo kwisha. Kwahiyo hawana sababu ya kukimbilia na kufanya vitendo vya uhalifu ambavyo mara zote vimekuwa na mwisho mbaya.

” Starehe haichakai wala haichuji, ipo na itaendelea kuwepo. Kila siku inaendelea kuwa mpya, yenyewe inakuchakaza na kukuzeesha wewe ukiendea kwa pupa. Kwahiyo hamna haja ya kukimbilia, ilikuwa, ipo na itaendelea kuwepo,” alionya Budi.

Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema serikali inalitambua vema kundi la vijana na mahataji yake. Kwahiyo imekuwa na mikakati mizuri yakulifanya lishiriki vizuri ujenzi wa uchumi wa nchi na vijana wenyewe. Hatahivyo baadhi ya vijana wanataka mafanikio ya haraka bila kufanya kazi halali kupitia mipango mizuri ya serikali ambayo ipo kwa ajili yao.

Budi ambae katika mahafali hayo alikabidhi seti mbili za jezi na mipira miwili kwa timu za mpira waa miguu na mikono( soccer & netball) za shule hiyo alitoa wito kwa wazazi kuwekeza kwenye elimu. Kwani ni mali isiyoibika na urithi usiogombewa na mtu yeyote.

Aidha Budi aliwakumbusha wazazi kutosahau wajibu wao wakuwafunza maadili mema, kufanya kazi halali na kuepuka vitendo vya uhalifu. Akibainisha kwamba jukumu la kudhibiti tabia lisiachwe kwa serikali bali watu wote.

Katika mahafali hayo ya 27 kwa shule ya sekondari ya Mnero tangu kuanzishwa yalikuwa na wahitimu 35. Kati ya hao, wahitimu 23 ni waschana na 12 wavulana.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *