img

Sheria ya India inayotishia mapenzi ya watu wenye imani za dini tofauti

December 12, 2020

Dakika 6 zilizopita

People from different human rights organizations hold placards during a protest against BJP-lead government and Chief Minister of Uttar Pradesh Yogi Adithyanath over the so-called "love Jihad" law,

Kila mwaka wanandoa wapatao 1,000 kutoka dini mbalimbali huwasiliana na kikundi cha Delhi cha usaidizi na kuomba msaada.

Wapenzi Wahindu na Waislamu mara kwa mara hukitembelea kikundi cha ushauri cha Dhanak wakati familia zao zinapokataa kuwapa ruhusa ya kuoana . Wengi wao huwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30 ,wanawake na wanaume walioolewa hutaka kikundi hiki kizungumze na familia zao au kuwasaidia kupata usaidizi wa kisheria.

Miongoni mwa wapenzi wanaofika katika kikundi cha Dhanak, 52% ni Wahindu wanawake wanaopanga kuolewa na wanaume wa Kiislamu, na 42% ni Waislamu wanawake Waislamu wanaopangha kuolewa na wanaume Wahindu.

” Familia za Wahindu na Waislamu wote hupinga vikali ndoa za watu wenye imani tofauti ,” Asif Iqbal, muasisi wa Dhanak, aliiambia BBC.

“Watatumia njia zote na kwa namna yoyote ili kuzuwia ndoa hizo. Wazazi huamua hata kuwaharibia sifa mabinti zao kwa kuwasemea mabaya ya uongo ili kuwakatisha tamaa wapenzi wa mabinti zao na kuhakikisha wanaharibu mahusiano ya binti zao .”

Jinamizi la “mapenzi ya jihadi “, neno ambalo linatumiwa na makundi ya Wahindu wenye itikadi kali ambao wanalitumia kuwashutumu Wanaume wa Kiislamu wanaowaingiza wanawake Wahindu katika Uislamu kwa kutumia ndoa, limerejea kuathiri mahusiano ya ndao za watu wa imani tofauti.

Wiki iliyopita , polisi katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh walimkamata mwanaume Muislamu kwa madai kuwa alikuwa kijaribu kumuingiza mwanamke Mhindu katika Uislamu – alikuwa ni wa kwanza kukamatwa chini ta sheria inayozuia kubadili dini inayolenga mapenzi -ya jihad.

Takriban majimbo mengine manne yanayoongozwa na Wahindu wa chama Bharatiya Janata yanapanga kuidhinisha sheria sawa na hiyo. Msemaji wa chama hicho alisema kuwa sheria zinahitajika ili kuzuia “udanganyifu, ufisadi na upotoshaji “.

“Wakati mwanaume wa dini ya Hindu anapomua mwanamke Muislamu, wakati wote inaonesha kama mapenzi ya dhati , lakini inapokuwa kwamba mwanamke Muislamu anaolewa na Muhindu inaonekana kama kulazimisha ,”anasema Charu Gupta, mwanahistoria katika Chuo Kikuu cha Delhi, ambaye alifanya utafiti juu ya “hadithi za mapenzi ya jihadi ” .

An Indian Hindu holds a placard as she takes part in a rally against 'Love Jihad', in Ahmedabad on July 22, 2018.

Maelezo ya picha,

Maandamano dhidi ya ‘mapenzi ya jihad’ katika jimbo la magharibi la Ahmedabad mwaka 2018

Mapenzi bado yanasalia kuwa kitu kigumu – na hatari -katika majimbo mengi ya India yenye mfumo dume , ufalme naheshima ya familia.

Bado vijana wa kike na kiume wa kutoka dini zote wamekuwa wakiishi maisha ya upinzani katika vijiji na miji midogo . Wakisaidiwa na simu za mkononi na data za intaneti za bei nafuu pamoja na mitando ya kijamii, wanakutana na kupendana kwa wingi kuliko ilivyokuwa awali.

Wanavunja kile mwandishi wa vitabu Arundhati Roy, alichosema katika kitabu chake cha riwaya cha Mungu wa vitu vidogo- God of Small Things, alichoelezea kama “sheria za mapenzi” ambazo “zinaainisha ni nani anayepaswa kupendwa…Na kwa vipi…na kwa kiwango gani “.

Ndoa za kupangwa za watu wa ukoo mmoja na jamii moja ni zaidi ya 90% kote nchini India . Ndoa za watu wa dini tofauti ni nadra sana. Utafiti mmoja uliweka kiwango cha ndoa hizo kwa zaidi ya 2%. Wengi wanaamini kuwa mapenzi ya jihadi hufufuliwa mara kwa mara na makundi ya Kihindu kwa ajili ya maslahi ya kiasa.

Wakati mwamko wa kidini katika miaka ya 1920 na 1930 , makundi ya Wahindu katika maeneo ya kaskazini mwa India yalianzisha kampeni dhidi ya “utekaji nyara ” wa Wahindu wanawake waliokuwa wakitekwa na wanaume Waislamu na kudai kurejeshwa kwa wake wa Kihindu.

Hadiya Jahan was born into a Hindu family, but converted to Islam and married a Muslim man

Maelezo ya picha,

Mwaka 2018, mahakama ilimruhusu Hadiya Jahan ambaye alislimu kuwa muislamu na kuolewa kwa mwanaume wa kiislamu kuishi na mume wake.

Kikundi cha Kihindu kiliundwa katika jimbo la United Provinces (sasa likiitwa Uttar Pradesh, jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini India ) ili kuzuwia Waislam kufanya kile walichodai ‘kuwateka nyara wanawake Wahindu. Mwaka 1924, Muislamu mmoja maarufu katika jiji la Kanpur alishutumiwa “kuteka na kumdanganya ” msichana Mhindu na kumlazimisha kuingia Uislamu . Kikundi cha Wahindu kilidai mwanamke huyo ”aokolewe” kutoka kwa mwanaume huyo Muislamu.

Kutekwa nyara kwa wanawake Wahindu ni swala ambalo lilijadiliwa hata katika bungeni India enzi ya ukoloni . Chama cha Indian National Congress, ambacho kwa sasa ndio chama kikuu cha upinzani, kilipitisha azimio lililosema “wanawake waliotekwa na kulazimishwa kuolewa lazima warejeshwe kwao, mazungumzo mengi hayana maana au umuhimu watu wanapaswa kupewa fursa ya kurejea katika maisha waliyoyachagua “.

Wakati India ilipogawanywa katika mataifa mawili mwezi Agosti mwaka 1947, watu milioni moja walikufa na wengine milioni 15 walisambaratika huku Waislamu wakikimbilia Pakistan, na Wahindu na Wasing walikwenda maeneo mengine .

Katika nyakati za hivi karibuni Makundi ya Wahindu yanayopigania maslahi ya kitaifa yameibuka tena na jinamizi la “jihadi ya mapenzi ” kabla ya uchaguzi ili kuvuruga kura . Wakati mmoja ilikuwa ni wakati wa uchaguzi wa jimbo wa Uttar Pradesh mwaka 2014.

Profesa Gupta anasema makundi ya Wahindu” yalianzisha kampeni ya propaganda “, wakitumia matangazo, tetesi na uvumi, dhidi ya “kile walichodai ni utekaji nyara na kuwaslimu wanawake wa kihindu unaofanywa na wanaume wa Kiislamu. Walidai kwamba Wanaume wa kiislamu wanawabaka na kuwalazimisha kuwaoa, kwa ajili ya kuwaingiza katika dini ya kiisalmu wakitumia mapenzi “.

The runaway couples live under police protection in shelter homes

Maelezo ya picha,

Wanandoa waliotoroka wakiishi chini ya ulinzi wa polisi katika makazi yanayolindwa na polisi

Kuna mambo yanayofanana kati ya kampeni za ‘Jihadi ya mapenzi za zamani na za sasa, wanasema wanazuoni. Lakini baada ya muda, kampeni hizo zimekuwa ni za kulazimisha zaidikwasabau zimekuwa zikiongozwa na Bchama tawala cha BJP.

“Kabla ya uhuru kampeni za aina hiyo zilizikwa katika kurasa za ndani za magazeti. Hapakuwa na vyama vikuu ao viongozi waliochochea uhasma wa aina hiyo . Lakini sasa kampeni hizi ziko katika kurasa za mbele za magazeti na serikali imekuwa ikihusika katika utekelezwaji wa sheria hizi . Mitandao ya kijamii na huduma za barua pepevinatumiwa kusambaza jumbe kwamba Wanaume wa Kiislamu wanawaslimu kwa nguvu wanawake wa Kihindu kwa kutumia ndoa ,” anasema Profesa Gupta.

Wengi wanasema kuslimu hutokea wakati wapenzi wanapoamua ndoa ya kidini ili “kuepuka” Kipengele maalumu cha sheria ya India kuhusu ndoa, ambacho kinaruhusu ndoa za watu wa dini tofauti tu iwapo watakuwa wametoa taarifa zinazohusu maelezo ya kibinafsi ya wanandoa kwa mamlaka miezi kadhaa kabla ya ndoa kufungwa. Kwa hiyo wapenzi wanaotaka kuoana huhofia kwamba familia zao zitaingilia na kuzuia ndoa kufungwa.

Kuanzishwa kwa sheria za kuzuia chaguo la watu kutoa idhini yao ya kuoana kama watu wazima wa dini tofauti kumeleta hali ya hofu ambapo wazazi wote na mamlaka wanaweza kuitumia kuwaonya wapenzi vijana waache kufunga ndoa.

Kwa upande mwingine, wanaume na wanawake zaidi na zaidi wanavunja miiko ya kidini inayowagawana na kuwapenda wenzi wao wa dini tofauti na kulazimika kutengana na familia zao. Wengi wanatafuta hifadhi katika mnyumba zinazoendeshwa na serikali wakati taifa lenyewe linjajaribu kuzuia ndoa za aina hiyo. “Mapenzi ni jambo linalokanganya na gumu nchini India ,” anasema Bw Iqbal.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Huenda mnazungumza lugha ‘tofauti ya mapenzi’.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *