img

Mwanamgambo wa Hezbollah Salim Ayyash afungwa maisha kwa kumuua Hariri

December 12, 2020

Mwanamgambo wa kundi la Hezbollah amehukumiwa vifungo vitano jela bela kuwepo mahakamani kwa kumuua Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Alipatikana na makpsa mapema mwaka huu kwa kuhusika na mauaji hayo.

Majaji katika mahakama maalum ya Lebanon iliyo na makao yake nchini Uholanzi (STL) wamesema Salim Ayyash alikuwa kiungo muhimu katika shambulio la bomu la Beirut mwaka 2005 lililomuua Hariri.

Waliwaondolea mashtaka wastakiwa wengine watatu, ambao kama Ayyash walishtakiwa bila kufika mahakamani.

Hezbollah imepinga kuhusika na kivyovyote na shambulio hilo, na majaji wamesema hakuna ushahidi unaohusisha viongozi wa kundi hilo la wanamgambo wa Kishia.

Mahakama hiyo maalum pia ilimpata Salim Ayyash na kosa la mauaji. Rafiq Hariri aliuawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga miaka 15 iliyopita

Rafik Hariri, ambaye alikuwa wa dhehebu la Kiislamu la Sunni, alikuwa bilionea na mfanyabiashara aliyehudumu kama Waziri Mkuu wa Lebanon mara tano kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1975hadi miaka ya 1990.

Muhula wake wa mwisho madarakani ulimalizika mwaka 2004, na baada ya hapo aliungana na upinzani bungeni na kuunga mkono wito wa kutaka Syria kuondoa vikosi vyake, ambavyo vilikuwa nchini Lebanon tangu mwaka 1976.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *