img

Manchester United kumenyana na Manchester City leo

December 12, 2020

 

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa hatua kwa hatua leo atapambana na Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.

Leo Desemba 12, Uwanja wa Old Trafford,  Manchester United itamenyana na Manchester City ikiwa ni Manchester Dabi itakayokuwa na ushindani mkubwa majira ya saa 2:30 usiku.

Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizi zimekutana mara 182 na leo inakuwa ni mara ya 183 tangu zianze kukutana na mara ya kwanza ilikuwa ni Novemba 12,1881.

Manchester United imeshinda  jumla ya mechi 76 na City imeshinda jumla ya mechi 54 na zimekusanywa jumla ya sare 52 na utakuwa ni wa 47 tangu Premier League ibadilishe mfumo mwaka 1992.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *