img

Kenya yaadhimisha miaka 57 tangu kupata uhuru

December 12, 2020

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi, Kenyatta alieleza hatua muhimu zilizochukuliwa na utawala wake tangu alipochukua hatamu za uongozi mnamo mwaka wa 2013.

Maadhimisho hayo yalijiri huku taifa hilo la Afrika Mashariki likikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, ambayo, wachambuzi wanasema, kwa kiasi kikubwa, imesababishwa na janga la Corona.

Kwa mara nyingine, Kenyatta alitumia fursa hiyo kutetea msukumo unaoendelea wa kutaka kuifanyia marekebisho katiba ya Kenya, akieleza kwamba ndiyo njia ya pekee ya kupunguza uhasama unaojitokeza kila kipindi cha uchaguzi.

“Hali ya taharuki inayoshuhudiwa kila baada ya miaka mitano na ishara wazi kwamba katiba yetu ina mapungufu,” alisema Rais Kenyatta.

Hata hivyo, aliongeza kwamba marekebisho hayo hayatatatua mizozo yote ya kikatiba nchini humo.

“Haya yatatakuwa marekebisho ya kwanza ya katiba ya 2010 na yanakusudiwa kuboresha katiba hiyo. Huu sio mwisho wa marekebisho kwani mengine yatafuata katika siku za usoni,” alisema.

Azma ya kuifanyia marekebisho katiba ya Kenya imekuwa ikiibua hisia mseto, baadhi ya wananchi wakiipinga kwa misingi kwamba nia yake kubwa ni kuongeza nyadhifa za uongozi kwa wachache na kwamba huu si wakati muafaka kwa sababu ya mazingira ya janga la Corona.

Wakati wa maadhimisho ya Jumamosi, Kenyatta alitangaza kwamba serikali yake iko tayari kuhakikisha kwamba wanafunzi wote watarejea shuleni tarehe 4 mwezi Januari mwakani, baada ya kuwa likizoni kwa takriban miezi tisa kwa sababu ya cahangamoto za janga la Corona.

Baadhi ya wanafunzi tayari wamerejea shuleni na vyuoni.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na naibu wa rais William Ruto, Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, Makamu wa rais wa zamani, Kalonzo Musyoka, na mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta kati ya wengine.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *