img

Hukumu ya kifo: Ni nchi ngapi ambazo bado zinatekeleza hukumu ya kifo?

December 12, 2020

 Hukumu ya kifo inagonga vichwa vya habari kwani Rais wa Marekani Donald Trump ametoa idhini yake ya kutekelezwa kwa msururu wa hukumu hiyo kabla ya kuondoka madarakani.

Alfred Bourgeois kutoka jimbo la Indiana ametangazwa leo anatarajiwa kuuawa katika siku mbili zijazo, akiwa ni mfungwa wa pili kuuliwa na serikali ya shirikisho baada ya kipindi kirefu . Alfred alimuua mtoto wake mdogo wa kike karibu miaka 20 iliyopita.

Tumeangalia ni nchi ngapi duniani ambazo bado zinatekeleza adhabu ya kifo

Takwimu rasmi hazipo nje ya China, ambako takwimu zinazohusiana na hukumu hiyo ni siri ya taifa, lakini shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linakadiria kuwa maelfu ya watu waliuliwa katika mwaka 2019 .

Ukiondoa China, nchi tatu ambazo zilihusika na hukumu za vifo kwa kiwango cha asilimia zaidi 80% o ni Saudi Arabia, Iraq na Iran.

Kulingana na idadi ya Amnesty, China imekuwa ikiendelea kuwauwa watu zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Shirika la Amnesty hukusanya takwimu kwa kutumia namba rasmi, ripoti za vyombo vya habari na taarifa wanazozipata kutoka kwa watu binafsi waliohukumiwa kifo na familia na ndugu zao.

Saudi Arabia ilikuwa ni nchi pekee katika orodha iliyotumia mbinu ya kukata kichwa kama njia ya kutekeleza adhabu ya kuu.

Njia nyingine ni pamoja na kumnyonga mtu kwa kumning’iniza kwenye kamba , kuchoma sindano ya sumu na kuua kwa kupiga risasi.

nchini Marekani, majimbo sita yaliekeleza hukumu ya kifo kwa kutumia sindano ya sumu mwaka 2019, na jimbo moja la (Tennessee) lilitumia umeme kuua.

Kwa ujumla watu 25 waliuawa nchini Marekani katika mwaka 2019, na kwa mwaka wa 11 Marekani imekuwa ndio nchi pekee iliyotekeleza adhabu ya kifo.

Tangu mwaka 2013, nchi 33 zilitekeleza hukumu ya kifo.

Ukiondoa China, mauaji utekelezwaji wa hukumu ya kifo umekuwa ukipungua tangu mwaka E 2015.

Hukumu za kifo 657 ezilirekodiwa mwaka 2019. Hiyo ni chini ya 5% ya zile zilizotolewa mwaka 2018, na idadi hiyo ni ndogo kuwahi kushuhudiwa kwa kipindi cha zaidi ya muongo.

Idadi ya nchi ambazo zilipiga marufuku adhabu ya kifo zimekuwa zikiongezeka , kuanzia nchi 48 katika mwaka 1991 hadi 106 mwaka 2017.

Hakuna nchi ya ziada iliyopiga marufuku adhabu ya kifo katika mwaka 2019 kwa mwaka wa pili mfulurizo , lakini Amnesty inasema kuwa nchi 142 hazijapiga marufuku hukumu ya kifo kisheria au kivitendo a

Takriban hukumu 2,307 za kifo ziliidhinishwa katika nchi 56 mwaka 2019. Lakini wakati mwingine hukumu za vifo zimekuwa zikiahirishwa , katika nchi ambazo zinasita kutekeleza adhabu hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni nchi ambazo zilitekeleza mauaji zimepungua

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *