img

Anthony Joshua: Ni kwanini Wanigeria wanamuona kama mmoja wao

December 12, 2020

Dakika 7 zilizopita

Anthony Joshua

Usiku wa Jumamosi katika jiji la London, Anthony Joshua ataingia ulingani kwa mara ya kwanza mwaka huu kupigana na Kubrat Pulev wa Bulgeria.

Kutokana na janga la corona ni mashabiki 1,000 pekee ndio watakuwa na bahati ya kushuhudia pigano hilo katika uwanja wa SSE Arena kumuona Joshua akipigania kuhifadhi taji lake la bingwa wa uzani wa juu mara tatu

Japo uwanja huo utakuwa na watu wachache, mamilioni ya watu watakuwa wanafuatilia piano hilo kwenye radio na televisheni huku raia wa Nigeria wakitarajiwa kumshabikia Joshua.

Mwana ndondi mwenye umri wa miaka 31- huenda ameshindia Uingereza nishani ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki, lakini ushindi huo unasherehekewa zaidi katika mji wa kusini – magharibi wa Sagamu, Nigeria ambako familia yake inatokea.

Alikoanzia

Familia ya Joshua inajulikana sana Sagamu ambako mababu walizaliwa.

Babu yake mkuu Daniel Adebambo Joshua, tajiri aliyemiliki ardhi na mfanyabiashara anasadikiwa kubatizwa jina lake mwisho baada ya kijiunga na dini ya Kikristo.

Daniel alimpelekwa mwanawe wa kiume Isaac Olaseni Joshua kwa msomo nchini Uingereza ambako hatimaye alioana na mwanamke kutoka Ireland na kurudi naye nyumbani Nigeria na kuzaa na kulea watoto saba pamoja.

Mmoja wa watoto hao, Robert aliishia kumuoa Yeta Odusanya, pia kutoka Sagamu, ambayeapia ni baba yake Anthony na dada yake Janet.

Jina lake la kati kati Olaseni alipewa kwa heshima ya babu yake. Shughuli zake za michezo hivi karibuni zimehakikisha jina la familia linakuwa maarufu sio tu katika mji huo bali pia ndani na nje ya nchi.

Showing off his heritage

Joshua anajivunia sana chimbuko lake la Nigeria mfano mzuri ukiwa mchoro wa attoo ya Afrika, ikiwa na benders ya Nigeria katika bega lake la kulia.

Bendera ya Nigeria huwa inapeperushwa pamoja na bendera ya muung Union Jack ndani ya ulingo wa mapigano.

Muziki uliochezwa wakati akiingia ulingoni katika mapigano yake mawili dhidi ya Andy Ruiz Jr. umekuwa wa wasani nyota wa Nigeria kama vile Burna Boy na Femi Kuti, mwana wa kiume wa nguli wa muziki wa Kiafrika Fela Kuti.

Mapenzi yake kwa muziki wa Nigeria yanaonekana katika mitandao yake ya kijamiii ambako anyone kana akiweka video yake akiimba nyimbo kutoka nchi hiyo ya Afrika magharibi .

Vitu vingine anavyopenda kutoka Nigeria ni vyakula vya kiasili ambavyo pia mara kadhaa hujivunia kuoneshana anavyojua kupika.

Upendo wa Joshua kwa Nigeria pia umemfanya kutuma misaada ya chakula
Maelezo ya picha,

Upendo wa Joshua kwa Nigeria pia umemfanya kutuma misaada ya chakula

Upendo wa Joshua kwa Nigeria pia umemfanya kutuma misaada ya chakula na bidhaa zingine muhimu kwa familia zilizoathiriwa na janga la corona.

Hivi karibuni aliandika ujumbe katika mitandao ya kijamii kusimama na vijana waliokuwa wakiandamana kupinga dharma za polisi bnchini Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ni shabiki, wawili hao walikutana mjini London mwezi Januari ambapo Joshua alimpatia mishipi yake.

Matukio haya yote yamemfanya kupendwa sana mashabiki wake Wanigeria ambao wanahisi ni mmoja wao kuliko wanandondi wengine wa uzani wa juu waliyokuwa na kizazi cha Nigeria waliyokuwa mbele yake.

Henry Akinwande na Samuel Peter wote walishinda mataji WBO na WBC siku zilizopita lakini hakuna hata mmoja wao anayemfikia Joshua kwa umaarufu nchini Nigeria.

Kando na hayo, Joshua ana klabubyake ya mashabiki mjini Sagamu ambayo alianzisha mwaka 2017 kabla ya piano lililoimarisha taaluma yake dhidi ya Wladimir Klitschko.

“Joshua ameiweka Sagamu kwenye ramani,” Azeez Adekunle Okunoren, aka Bwana Naira, mwanzilishi wa klabu ya mashabiki wa Anthony Joshua, aliambia BBC michezo Afrika.

“Katika piano lake la mwisho dhidi ya Andy Ruiz, tulionesha piano hilo kwa umma kwenye spring kubwa kwa kutumia projector.

“Mashabiki karibu 10,000 walijitokeza kutazama pigano hilo. Baadhi yao walisafiri kutoka miji jirani kujionea.

“Hata sasa tumepokea simu nyingi kutoka kwa watu wanaotaka kujua kama tutaonesha pigano la Joshua la leo usiku dhidi ya Pulev.”

Antony Joshua akiwa na baba yake baada ya kumchapa Carlos Takam
Maelezo ya picha,

Antony Joshua akiwa na baba yake baada ya kumchapa Carlos Takam

Kuangaziwa na vyombo vya habari

Televisheni, Radio, Magazeti na Tovuti zote nchini Nigeria zinatoa muda na nafasi kubwa kuhusu mapigano yake na maandalizi kuelekea mapigano hayo

Licha ya kwamba Joshua hajawahi kukutana na mashabiki wake na hata ilipozuru Sagamu mwezi Februari mwaka huu na kuamua kukutana na viongozi wa kijamii na kuondoka kimya kimya alivyokuja , watu hakumchukulia vibaya.

“Haijalishi. Yeye bado ni mtoto wetu na mwakilishi wetu,” anasema Okunoren.

“Baba yake, babu yake na babu wa mababu zake wanatoka hapa. Najua pia ana mizizi mjini Watford lakini hakuna namna tutakoza kumuunga mkono. Tunaamini siku moja atatutambua na kutusaidia.

“Tutazidi kumuombea apate ufanisi lakini pia tunataka uwepo wake hapa. Tungelipenda avenge nyumba hapa au kuwacha ishara yake hapa.

“Iwe ni kituo cha mazoezi ya viungo, au hospitali. Kitu ambacho watu Watson na ambacho kitawakumbusha kumhusu.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *