img

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Albania ajiuzulu

December 11, 2020

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Albania Sandër Lleshaj ametangaza kujiuzulu kufuatia maandamano yaliyoendelea nchini.

Waziri Mkuu Edi Rama alitangaza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliwasilisha ombi la kujiuzulu  baada ya kijana mmoja kupigwa risasi na kuuawa kwa kukosa kutii onyo la polisi katika mji mkuu, wa Tirana nchini humo.

Maandamano ya kupinga mauaji ya kijana huyo aliyefariki hospitalini baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa na polisi yaliendelea hapo jana.

Watu wengi wakiwemo wanaharakati wa asasi za kiraia, walikusanyika mbele ya ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kutoa kaulimbiu ya  “Hakuna haki, hakuna amani.” Waandamanaji waliwarushia polisi mawe na vitu vingine. Polisi kadhaa walipewa jukumu la kulinda majengo ya taasisi.

Wakati maandamano hayo yalipokuwa yakiendelea, Waziri Mkuu Rama alitoa taarifa na kutangaza kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani Lleshaj amewasilisha ombi la kujiuzulu.

Katika maandamano hayo yaliyofanyika mbele ya ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani na jengo la Waziri Mkuu siku iliyopita kwa kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ajiuzulu, maafisa 16 wa polisi, mfanyikazi 1 wa usalama na raia kadhaa walijeruhiwa.

Kijana K.R mwenye umri wa miaka 25 aliyepigwa risasi baada ya kukosa kutii amri ya polisi waliomuamuru asimame nyakati za marufuku ya kutoka nje mwendo wa saa 01.45 mnamo Desemba 8 katika mji mkuu wa Tirana, alijeruhiwa na baadaye akafariki kwenye hospitali aliyopelekwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *