img

Wanajeshi 1000 waliotekwa na waasi waokolewa Ethiopia

December 11, 2020

Wanajeshi wapatao 1000 akiwemo jenerali mmoja, wameokolewa kufuatia operesheni ya pamoja iliyoendeshwa na vikosi vya kijeshi na polisi nchini Ethiopia.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Mohammed Tessema,  alisema kwamba wanajeshi walichukuliwa mateka kwa wingi wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa Novemba 3 ambapo mashambulizi ya kambi ya Kaskazini yalitekelezwa na vikosi vya waasi wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF) na Jenerali Brigedia Adamneh Mengiste alikuwa miongoni mwa waliotekwa.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa maelfu ya watu walipoteza maisha na karibu watu 50,000 walitorokea mafichoni nchini Sudan kutokana na operesheni ya kijeshi iliyozinduliwa na jeshi la kitaifa la Ethiopia mnamo Novemba 4 baada ya mashambulizi ya TPLF.

Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yanasubiria idhini ya serikali ya Addis Ababa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika maeneo ambayo maelfu ya watu wameathirika na kuhama makazi yao kutokana na mizozo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza wiki iliyopita kwamba awamu ya mwisho ya operesheni hiyo ilikamilishwa baada ya kukombolewa kwa mji mkuu wa jimbo la Mekelle, na wahalifu watakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *