img

Wanafunzi wa Tanzania 30 kufadhiliwa masomo Hungary 2021/23

December 11, 2020

Tanzania na Hungary zimetiliana saini ya makubaliano ya ufadhili kwa wanafunzi zaidi ya 30 wa Kitanzania kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nchini Hungary katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2023.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Hungury, Dkt. Abdalla Possi amesema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa wanafunzi wa Tanzania kupata elimu katika vyuo vya Hungary kwa masomo ya shahada ya kwanza, shahada ya Uzamili na shahada ya uzamivu katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Hungury na kwamba nafasi hizo zitaendelea kuongezeka kutokana na Serikali ya Hungary kufurahishwa na muitikio wa Watanzania wanaoomba nafasi hizo za masomo.

Wakati huo huo Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani umefungua rasmi Ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika mji wa Bruno nchini Jamhuri ya Czech.

Tanzania imemwidhinisha Roman Grolig kuwa mwakilishi wa heshima wa Tanzania katika nchi hiyo ya Czech ambapo mji wa Bruno ni mji wa kimkakati ambapo kila mwaka mamlaka za mji huo huandaa miongoni mwa mambo mengine maonesho makubwa ya biashara na utaliibarani Ulaya.

Mji wa Bruno pia ni makao makuu ya Baraza la Biashara la Czech – Tanzanis

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *