img

Uganda yaagiza dozi milioni mbili za chanjo ya Covid-19

December 11, 2020

Uganda imeomba dozi zaidi ya milioni mbili za chanjo ya covid wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka katika taifa hilo na kufikia 25,000.

‘’Wazara imeomba chanjo ya Covid-19 ya AstraZeneca kupitia shirika la Global Vaccine Alliance (GAVI) na kuwa mchakato uko kwenye hatua za kuelekea mwishoni ,’’Ripoti ya tovuti moja binafsi imemnukuu Mkurugenzi wa huduma za afya, Henry Mwebesa, akiongea.

‘’Hii ni chanjo (AstraZeneca) ambayo serikali inatambua imepatiwa idhini na Shirila la Afya Duniani.. ni muhimu kufahamu kwamba chanjo inayopitishwa na Wizara ya Afya na WHO ndio inaweza kutumika na raia wa Uganda,’’ aliongeza Dkt Mwabesa.

Uganda inatarajia kupokea dozi milioni mbili kutoka Gavi mwanzoni mwa mwaka 2021 lakini “inatenga bajeti kwa ajili ya kunua dozi zaidi kwa ajili ya raia wa Uganda’’.

Kumekuwa na ongezeko la maamukizi kila siku wakati ambapo taifa hilo linajiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 14 mwezi Januari 2021.

Baadhi ya wanasiasa wameshutumiwa kukiuka masharti ya kudhibiti virusi vya corona wakati wa kampeni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *