img

Ufaransa yarefusha muda wa vizuizi vya kuzuia kuenea virusi vya corona

December 11, 2020

Ufaransa imetangaza kuahirisha hatua yake ya kulegeza vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona kwa kile kilichoelezwa kuwa taifa hilo halijafikia kilele cha wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo.

Waziri mkuu wa Ufaransa Jean Castex ambaye amesema majumba ya makumbusho, kumbi za sinema na maonesho vitaendelea kufungwa hadi mwezi Januari mwaka ujao.

Kadhalika chini ya uamuzi huo marufuku ya kutembea usiku itaendelea kutekelezwa ikiwemo siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Hapo kabla Ufaransa ilinuwia kuondoa vizuizi hivyo mwanzoni mwa mwezi Disemba lakini taifa hilo limeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la maambukizi mapya ya virusi vya corona.

Ufaransa ni moja ya mataifa yaliyoathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona na jana ilirikodi maambukizi mapya 14,600 huku idadi ya waliokufa ikifikia jumla ya watu 56,000.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *