img

Timu za uratibu za Konga wapigwa msasa juu ya usimamizi wa fedha

December 11, 2020

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Ili kufikia malengo na kupata matokeo chanya dhidi ya kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwa (VVU) katika jamii,makalani wa konga 15,viongozi 30 pamoja na waratibu wa ukimwi (CHAC) 15 wanaofanya jumla ya wajumbe 60 kanda ya  Mbeya wamefanikiwa kupata mafunzo ya usimamizi wa fedha yatakayowawezesha kusimamia vema rasilimali fedha wakati wa majukumu yao.

Lustika banzi ni katibu wa konga manispaa ya Iringa,amesema ili kusimamia vema rasilimali fedha zinazotolewa na wafadhili katika mapambano dhidi maambukizi ya VVU.Wanaamini mafunzo hayo yanayotolewa mkoani Njombe kupitia mradi wa Hebu Tuyajenge unaotekelezwa na baraza  la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (NACOPHA) kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la watu wa Marekani (USAID),yatawasaidia katika kuendeleza mapambano hayo.

“Tuko Njombe kwa ajili ya mafunzo ya usimamizi wa fedha na mafunzo haya yanalenga fedha zilizotolewa na ufadhili wa watu wa Marekani kutoka mradi wa hebu Tuya Jenge katika kutekeleza shughuli mbali mbali,tunaimani kabisa mafunzo yatatusaidia ili kutekeleza vizuri majukumu yetu ya kuhamasisha jamii kupima VVU,kurudisha watoro wa Dawa,kuhamasisha wenza na familia zao kupima VVU pamoja na kuhamasisha WAVIU kupima uwingi wa VVU”alisema Lustika banzi

Kibuga Fute ni mwenyekiti wa konga ya  halmashauri ya wilaya ya Mufindi na John Msoph ni katibu wa konga ya halmashauri ya mji wa Njombe,wamesema mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia kuwafikia walengwa wengi zaidi ambao bado hawajajua hali zao na kushawishi kuwatambua afya zao.

“Yatanisaidia kwenda kuwashawishi wengi zaidi ambao hawajajua hali zao za maambukizi kwasababu kwenye jamii tunao watu wengi ambao bado hawajajua hali zao hususani kwa kuwa shudia afya yangu”Alisema Kibuga Fute

Naye John Msoph alisema “Nimefanikiwa kuwa na mwenza ambaye hana virusi vya ukimwi na mimi ninaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi toka mwaka 2015 nikiwa darasa la tano na tumeweza kuzaa watoto ambao hawana virusi vya ukimwi,ninaamini kupitia mafunzo tunayoendelea nayo tutapata uwezo zaidi wa kwenda kutoa elimu lakini niwaomba vijana wenzangu waweze kutambua hali zao za maambukizi ikiwa bado wana nguvu”alisema John Msoph alisema

Catherin Ulaya ni meneja wa mradi wa Hebu tuyajenge kanda ya Mbeya,amesema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano 2019-2024 kwa kushirikiana na wadau wane katika halmashauri 15 za kanda ya mbeya huku ukiwa na malengo kadhaa ikiwemo kuimiza jamii kuongeza utumiaji sahihi wa huduma za ukimwi katika maeneo ya kinga,tiba,matunzo kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU hasa wasichana baleen a wanawake wa umri wakati pamoja na WAVIU katika halmashauri 65 nchini.

“Lakini pia lengo letu mahususi la kwanza ni kuongeza matumizi ya huduma ya upimaji,tiba na uzazi wa mpango kwa vijana na WAVIU lakini pia kuimarisha mashirika na miundo ya taasisi za WAVIU”alisema Catherin Ulaya

Kwa upande wake Dkt,Bumi Mwamasage mganga mkuu wa mkoa wa Njombe aliyekuwa mgeni wa heshima katika ufunguzi wa mafunzo hayo amewataka wajumbe hao kuzingatia mafunzo kwa usimamizi wa fedha kwa kuwa kipengere cha fedha kimekuwa kikileta migogoro katika makundi ya watu.

“Hii semina pia inahusisha mipango ya bajeti ile mipango inatakiwa iakisia hali halisi ya kule tunakotoka na vile vipaumbele vinavyopelekea kutimiza malengo yetu ndivyo vinavyotakiwa kuakisi kwenye bajeti zetu,na tukienda kinyume tutajikuta hatufanyi kitu cha maana”alisema Dkt Bumi Mwamasage.

Vile vile amewataka wajumbe hao kwenda kuongeza nguvu ya kuhamasisha wadau kwenda kupima afya zao kwa kuwa mradi huo umekuwa chachu kwa kufanya kazi na halmashauri nyingi zikiwemo zote sita za mkoa wa Njombe huku wakiwa na malengo mahususi sawa na serikali.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *