img

Serikali ya Ethiopia yatuma shehena ya nafaka jimboni Tigray

December 11, 2020

Serikali ya Ethiopia imesema jana kuwa imetuma shehena ya ngano kwenye jimbo la Tigray katika wakati mzozo unaoendelea umezuia karibu mashirika yote ya misaada ya kiutu kulifikia jimbo hilo.

Shirika la habari la FANA limeripoti kuwa msafara wa malori 30 uliwasili jana kwenye mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele na kwamba matayarisho ya kusambaza msaada huo wa chakula yanaendelea.

Makubaliano ya wiki iliyopita ya kuuruhusu Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya msaada kulifikia jimbo hilo yameshindwa kutekelezwa, hatua iliyoibua wasiwasi wa kimataifa juu ya hali ngumu itakayowakabili raia na wakimbizi.Jimbo la Tigray lipo kwenye mzozo tangu waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipoamuru mwanzoni mwa mwezi Novemba kufanyika operesheni ya kijeshi dhidi ya viongozi na wapiganaji wa chama cha TPLF kinachoongoza jimbo hilo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *