img

Morocco kurejesha mahusiano na Israel

December 11, 2020

Kumekuwapo na kauli mchanganyiko tangu Morocco na Israel kutangaza makubaliano ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia, baada ya Marekani kutangaza kuitambua Sahara Magharibi kuwa ni sehemu ya Morocco hapo jana. 

Wakati Rais Abdul Fattah al Sisi wa Misri ameipongeza hatua hiyo, chama cha Hamas kwenye Ukingo wa Gaza imeiita kuwa ni usaliti kwa dhamira ya Wapalestina, huku chama cha Polisario kinachopigania uhuru wa Sahara Magharibi kikiilaani vikali Marekani kwa kuizawadia Morocco haki isiyokuwa yake.

 Morocco linakuwa taifa la nne la Kiarabu ndani ya kipindi cha miezi minne, kuachana na msimamo wa miongo kadhaa wa kuitenga Israel, ikitanguliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan.

Kampeni ya kuyashawishi mataifa ya Kiarabu kukurubiana na Israel inaongozwa na Marekani, ikiwa kama njia ya kuunda muungano wa kukabiliana na kumkomowa hasimu wake mkubwa, Iran.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *