img

Kiongozi Mkuu wa Iran: Ni nani huenda akamrithi Ali Khamenei?

December 11, 2020

Dakika 5 zilizopita

Ayatollah Ali Khamenei speaks in Tehran, Iran, on 3 November 2020

Uvumi wa hivi karibuni juu ya afya ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, umetupa angalizo juu ya nini kitatokea ikiwa atakuwa mgonjwa sana kutawala, au kufa.

Kiongozi huyo mweye umri wa miaka 81- ana mamlaka ya juu zaidi ya kisiasa katika nchi za Mashariki ya kati, kuashiria kwamba mrithi wake atakuwa na umuhimu mkubwa kwa Iran, kanda nzima ya na ulimwengu kwa ujumla

Kiongozi Mkuu huchaguliwaje?

Anayeshikilia wadhifa huo (Ayatollah Khamenei ndiye kiongozi wa pili tangu mapinduzi ya Kislamu ya Iran mwaka 1979) huteuliwa na baraza la viongozi 88 wa kidini linalojulikana kama baraza la wataalamu.

Wanachama wake huchaguliwa na raia wa Iran kila baada ya miaka minane, lakini wagombea kwanza wanaidhinishwa na kamati maalumi inayofahamikama Baraza Mlezi. Wanachama wa Baraza hilo wenyewe wanateuliwa moja kwa moja na Kiongozi Mkuu au kupitia ushawishi wake.

Kiongozi Mkuu kwa hivyo ana ushawishi dhidi ya mabaraza yote mawili. Katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, Ali Khamenei amehakikisha wadhafidhina wanachaguliwa katika bunge hilo ili kuhakikisha anafuata nyayo ya mtangulizi wake.

Members of Iran's Assembly of Experts attend a session in Tehran on 12 March 2019

Maelezo ya picha,

Baraza la wataalamu humteua Kiongozi Mkuu na – kinadharia – linaweza kumuondoa

Anapochaguliwa, Kiongozi mkuu huenda akashikilia wadhifa huo daima.

Kwa mujibu wa katiba ya Iran, Kiongozi Mkuu sharti awe ayatollah, kiongozi wa ngazi ya juu katika dhehebu la Kishia. Lakini Ali Khamenei was alipochaguliwahakuwa ayatollah, kwa hivyo sheria ilibadilishwa ili kumwezesha kukubali kazi hiyo

Kwa hivyo, huenda sheria ikabadilishwa tena, kulingana na mazingira ya kisiasa ya wakati kiongozi mpya atachaguliwa.

Kiongozi Mkuu ana mamlaka ya mwisho nchini Iran. Anatoa uamuzi wa mwisho kuhusu masuala muhimu, utungaji wa sera na jinsi nchi inavyoshirikiana na mataifa mengine ulimwenguni.

Iran ni nchi ya Kishia iliyo na mamlaka makubwa duniani na chini ya uongozi wa Ali Khamenei imeimarisha na kupanua ushawishi wake Mashariki Kati.

Iranian Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei (R3), Quds Force commander Gen Esmail Qaani (R2), Iranian President Hassan Rouhani (R4), Judiciary chief Ebrahim Raisi (L4), chairman of the Assembly of Experts Ahmad Jannati (R) attend a memorial for Qasem Soleimani in Tehran, Iran on 9 January 2020

Maelezo ya picha,

Kiongozi Mkuu yuko juu katika muundo wa nguvu ya kisiasa ya Iran

Kifo chaka huenda isibadilishe mkondo wa kihistoria katika kanda hiyo lakini pia athari yake huenda ikatikisa dunia.

Uhasama kati ya Iran na Marekani na Israel, kwa mfano – ilichangiwa zaidi na kiwango cha chuki binafsi cha Ayatollah Khamenei dhidi ya pande hizo mbili – hali ambayo imechangia mtafaruku wa miaka kadhaa na kuyumba kwa taifa hilo.

Hata hivyo, mchakato wa wa kumtafuta mrithi unaadhiri akuwa yeyote atakayechukua nafasi yake huenda akafuata nyayo zake.

Nani hunda akawa Kiongozi Mkuu anayefuata?

Vitengo vya kisiasa vya nchi hiyo ya Kiislamu vina vina maslahi makubwa katika uamuzi wa kiongozi ajaye wa wadhifa huo, lakini hakuna mtu aliye na uwezo wa kufikia uamuzi huo ili kuepusha mgogoro.

Japo hakuwa na ushawishi mkubwa kama mtangulizi wake, Ali Khamenei ameimarisha ushawishi wake kupitia mtandao wake binafsi wa washirika watiifu, wengi wao katika kikosi kilicho na uwezo mkubwa cha Revolutionary Guards.

Iranian Revolutionary Guards commander Major General Hossein Salami speaks during a pro-government rally in Tehran on 25 November 2019

Maelezo ya picha,

Jeshi la Iran, linaloongozwa na Meja Jenerali Hossein Salami, lina uwezo mkubwa wa wa kijeshi , kisiasa na kiuchumi nchini Iran

Kuna uwezekano Jeshi la Iran linaweza kumzuia wagombea wowowte yote wanaowapinga kuwa Kiongozi Mkuu mpya.

Japo kumekuwa na uvumi kwamba kuna orodha ya siri iliyo namajina ambayo hayajulika – na hakuna mtu aliye dai kujua waliojumuishwa katika orodha hiyo.

Ripoti zinasema kuwa mgombea anayependelewana Ali Khamenei huenda kawa mwanawe wa kiume Mojtaba au Mkuu wa Idara ya Mahakama Ebrahim Raisi – ambazo kama ni kweli huenda zikawa na uzito.

Mrithi wa Bwana Raisi, Sadeq Larijani, na rais wa sasa Hassan Rouhani pia wanaaminiwa kutaka kuwa Kiongozi Mkuu.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *