img

Jinsi maafisa wa ngazi ya juu walivyolemaa na kuzirai wakati wa kesi za ufisadi Nigeria

December 11, 2020

 

Jinsi maafisa wa serikali ya Nigeria wanavyobadilika ghafla muonekano wao na kupata matatizo ya afya ghafla wakati wanapohojiwa kuhusiana na tuhuma za ufisadi sio suala geni nchini Nigeria.

Wanasiasa au maafisa wa ngazi ya juu wamekuwa wakitoweka kutoka ndani ya mahakama , na wengine wamekuwa wakifika mahakamani wakiwa katika viti vya walemavu au vya wagonjwa – wheelchairs kuomba msamaha au kutaka maelewano.

Wengi wanashutumiwa kwa ubadhilifu wa mali ya umma au ufisadi.

Katika tarifa hii tmewaangazia maafisa sita wa ngazi ya juu wa serikali ya Nigeria ambao wamegeuka na kuwa walemavu, kuanguka mahakamani baadhi hata kufa au kuugua wanapohojiwa kuhusiana na tuhuma dhidi yao.

Abdulrasheed Maina

Mwenyekiti wa zamani wa Hazina ya taifa ya akiba ya uzeeni nchini Nigeria , Abdulrasheed Maina, ambaye kesi yake imekuwa ikiendelea tangu mwaka 2019, amefariki ndani ya mahakama mjini Abuja baada ya kufika mbele ya mahakama hiyo jana Alhamisi.

Maina alihukumiwa kifungo cha maisha jela na jaji wa mahakama ya wilaya kwa madai ya ubadhilifu wa mali ya umma wa kiasi cha dola bilioni 2.

Video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii Bw Maina akitafuna ulimi wake huku akipata tena fahamu baada ya kuanguka na kuzirai.

Maina alikamatwa hivi karibuni katika Jamuhuri ya Niger ambako alirejeshwa nchini Nigeria na polisi ya kimataifa kuendelea na kesi yake baada ya kutoraka alipopewa dhamana.

Maina anashitakiwa na tume ya maendeleo ya uchumi EFCC mashitaka 12 , ikiwa ni pamoja na umiliki wa mali za gharama kubwa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Kamishina wa zamani wa Nigire Delta

Mwenyekiti wa Ushirika wa kimaendelea wa jimbo la Niger Delta (NDDC) alipata ulemavu wa ghafla wakati wa uchunguzi wa madai ya ubadhilifu wa mali uliofanywa na shirika lake.

Ulemavu huu ulitokea wakati wa kesi yake mwezi wa Julai 2020, wakati alipokuwa akiwaeleza wabunge wa kamati ya bunge la shirikisho inayohusika na masuala ya Niger Delta kuhusu jinsi kamati yake ilivyotumia mabilioni ya pesa za Nigeria -Naira.

Pondei alishindwa kupumua, akalala kwenye kiti. Hatimae alitolewa kwa mabavu nje ya chumba cha mkutano na wabunge waliokuwa na hasira huku wengine wakiupanua mdomo wake ili kuhakikisha kama kweli alikuwa amezirai au la. Matokeo yake, uchunguzi dhidi yake ulicheleweshwa kwa muda.

Bw Pondei pia alitoka nje ya uchunguzi huo bila kukamilika,akimshutumu mwenyekiti wa tume, seneta Olubunmi Tunji-Ojo kwa ufisadi.

Msemaji wa zamani wa chama cha PDP Olisa Metuh

Msemaji wa zamani wa chama cha PDP Olisa Metuh, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela, alionekana mara moja akiwa katika kitanda cha hospitali.

Alikamatwa akishukiwa kwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma wa Naira milioni 400kutoka katika mfuko wa zamani wa mshauri rais wa masuala ya usalama wa taifa , kanali Sambo Dasuki wakati wa utawala wa Rais Goodluck Jonathan.

Taasisi ya uchumi ya Nigeria EFCC, imefungua mashitaka dhidi yake.

Senata Dino Melaye

Polisi walimshutumu Seneta Senator Melaye kujaribu kuutoa uhai wake baada ya kuruka kutoka kwenye gari la polisi.

Senata Dino Melaye pia alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Abuja, wakati polisi wakitoa ushahidi dhidi yake.

Alifikishwa mahakamani na polisi waliomshitaki kujaribu kujiua na pia kujaribu kutoroka kutoka kwenye mahabusu yao mwaka 2018.

Makabiliano kati ya Dino Melaye na polisi yaliwavutia Wanigeria wengi wakati huo.

Gavana wa zamani Ayo Fayose

Gavana wa zamani wa Ekiti Ayo Fayose pia ameonesha dalili za kuugua katika makabiliano yake na vikosi vya usalama.

Fayose alionekana wakati mmoja akiangua kilio na kupiga mayowe akidai kuwa alipigwa na afisa wa polisi wakati wa uchaguzi wa gavana wa jimbo la Ekiti.

Ayodele Fayose, ambaye ni gavana wa jimbo la Ekiti lililopo kusini mwa Nigeia kutoka chama cha Peoples Democratic Party (PDP), amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Buhari.

Gavana huyo wa zamani anafahamika sana nchini Nigeria kwa ufisadi uliokithiri.

Waziri wa zamani wa ulinzi Bello Halliru

Kiongozi wa zamani wa chama cha PDP na waziri wa zamani wa Bello Haliru Mohammed wakati mmoja alionekana kwenye kiti cha walemavu au cha wagonjwa katika Mahakama ya juu ya Shirikisho nchini Nigeria mwaka 2016 wakati wa kesi dhidi yake.

Tume ya masuala ya kiuchumi EFCC inamshutumu kukubali dola bilioni 2 kwa mshauri wa zamani wa rais Sambo Dasuki, ambazo Dasukin aliiambia mahakama kuwa zilikuwa zimepangiwa kununulia silaha.

Na Bello Halliru wakati huo alifika mahakamani katika kiti cha walemavu, akidai kuwa alikuwa hana afya nzuri.

Kuna wanasiasa wengi nchini Nigeria ambao husingizia kuwa wana matatizo ya kiafya ili kuepuka kwenda mahakamani.

Baadhi yao ni pamoja na gavana wa jimbo la Adamawa Bala Ngilari, Waziri wa zamani wa masuala ya safari za ndege Femi Fani-Kayode na waziri wa zamani wa mafuta Diezani Alison-Madueke.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *