img

“Ipo siku nitakuwa Rais wa Tanzania” – Haji Manara

December 11, 2020

 

Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ametoa kali ya mwaka kwa kusema Mungu akimpa uhai na majaliwa ataenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka ijayo ila bado hajajua itakuwa lini.

Akifunguka hilo wakati anapiga stori na PlanetBongo ya East Africa Radio Haji Manara amesema kwa mfano akiwa Rais mtaji wake wa kwanza ukiacha masuala ya siasa na kazi za maendeleo ni kuwekeza kwenye mpira wa miguu.

“Mungu akinipa uhai na majaaliwa, chukueni haya maneno yangu leo, naenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mungu anipe uhai tu, sijui ni lini ila nitakuwa tu”

“Hakuna kitu kinachopendwa Tanzania kama michezo hasa mpira wa miguu, kwa mfano mimi nikiwa Rais mtaji wangu wa kwanza nje ya siasa na kazi za maendeleo nitawekeza kwenye mpira wa miguu” amesema Haji Manara 

Aidha amendelea kusema “Yanga na Simba zikishinda watu wanakimbia maandamano bila ya kulipwa au kuvalishwa fulana, angalia Simba tunapoenda mikoani ile sapoti tunayopata kwa mashabiki hata nikipata fursa ya kuzungumza na Rais nitamuachia maneno hayo”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *