img

IGP Sirro afunga mafunzo ya kikosi maalum cha Polisi

December 11, 2020

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka askari wa Jeshi hilo kuendelea kufanya mazoezi katika maeneo yao ya kiutendaji na hasa kujihusisha na mafunzo yatakayosaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Kikosi maalum cha Polisi cha ulinzi wa amani (Formed Police Unity) yaliyofanyika katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Naye mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo Rienada Milanzi, akitoa neno la shukurani mbele ya Mkuu wa Jeshi hilo amesema kuwa, wataendelea kuyatumia kwa vitendo na kwa ufasaha mafunzo waliyoyapata na kutoa matokeo chanya na yenye afya kwa Jeshi hilo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *