img

Haji Manara afunga ndoa, apewa neno

December 11, 2020

 

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, usiku wa kuamkia leo Desemba 10, amefunga ndoa na mkewe Naheeda, katika msikiti wa Masjid Maamur.
 Ndoa yake imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum na watu wengine wengi maarufu.
Kikwete amesema kuwa Haji alimfuata nyumbani na kumshirikisha jambo hilo kwa ajili ya ndoa na akamuahidi kuja.
Kikwete amesema:”Hakuna ufundi kwenye ndoa kikubwa ni kustahimiliana na kuvumiliana kwa kuwa hakuna ufundi katika ndoa.
“Mnapaswa kuwa makini na kuskilizana katika ndoa, pia nakushauri ujue kwamba uwe na uvumilivu na kuona namna gani mnaweza kuleta watoto kwa kuulizana na kujua mambo yatakuaje.
“Baraka za Mungu kwa watoto ni zake ka kadri atakavyoamua, yale makundi yaache kwa kuwa kila mmoja anajua anachokipenda.
“Nilikuwa ninazungumza na mzee hapo nyuma akaniambia kwamba anahitaji wajukuu hivyo ni jambo la kheri na linahitaji subira kikubwa ninawapongeza katika hilo na ninaamini kwamba itakuwa kheri,” amesema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *