img

Brandon Bernard: Hukumu ya kuuawa kwake katika siku za mwisho za Trump madarakani

December 11, 2020

Dakika 4 zilizopita

Brandon Bernard

Hukumu ya kifo ya mfungwa Brandon Bernard imetekelezwa jimboni Indiana baada ya ombi la dakika za mwisho kutenguliwa kwa hukumu kukataliwa na Mahakama kuu ya Marekani

Bernard mwenye miaka 40, alihukumiwa kwa makosa ya mauaji mwaka 1999 alipokuwa kijana mdogo, na alikuwa mhalifu mdogo kuhukumiwa na serikali katika kipindi cha miaka karibu 70.

Bernard aliiambia familia ya wenza aliowaua kuwa anaomba msamaha, kabla ya kuuawa kwa kuchomwa sindano siku ya Alhamisi.

Hukumu nyingine nne za vifo zimepangwa kutekelezwa kabla Donald Trump hajaondoka madarakani.

Ikiwa yote matano yatafanyika, Bwana Trump atakuwa amesimamia hukumu zaidi za kifo katika kipindi cha zaidi ya karne moja. Na kufanya idadi yake kufikia 13 tangu mwezi Julai.

Maneno yake ya mwisho kabla ya kifo

Bernard alitangazwa kuwa amekufa saa 21:27 za huko siku ya Alhamisi sawa na saa 11 siku ya Ijumaa katika gereza la jela la Terre Haute.

Kabla ya hayo alielekeza maneno yake ya mwisho kwa familia ya walioathirika, akizungumza kwa utulivu kwa zaidi ya dakika tatu.

”Ninaomba radhi. Haya ni maneno pekee ninayoweza kusema kuelezea namna ninavyojisikia sasa na namna nilivyojisikia siku hiyo,” alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.

Utekelezaji wa hukumu ya kuuawa ulicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili baada ya mawakili wa Bernard kuitaka Mahakama kuu kusitisha- lakini ombi hilo lilikataliwa.

Bernard alipewa adhabu ya kifo kwa kuhusika kwake katika mauaji ya Todd na Stacie Bagley mnamo Juni 1999.

Alikuwa mmoja wa vijana watano wanaotuhumiwa kuwaibia wawili hao na kuwalazimisha kuketi nyuma ya gari lao huko Texas.

Walipigwa risasi kwenye gari na mwenzao wa miaka 19 Christopher Vialva kabla ya Bernard kulichoma moto gari.

Mawakili wa utetezi wanasema wote wawili walifariki kabla ya gari kuchomwa moto.

Mchunguzi huru aliyeajiriwa na upande wa utetezi alisema Stacie alikuwa amekufa kabla ya moto.

Walakini, ushuhuda wa serikali wakati wa kesi hiyo ulidai kwamba ingawa Todd Bagley alikufa papo hapo, Stacie alikuwa na masizi katika njia yake ya hewa, akiashiria kwamba alikufa kutokana na kuvuta pumzi ya moshi na sio jeraha la risasi.

Mawakili wa Bernard wanadai aliogopa nini kingetokea kwake ikiwa atakataa kufuata maagizo ya Vialva, ambaye aliuawa mnamo Septemba.

Wengine waliohusika katika tukio hilo walipewa vifungo vya gerezani kwani walikuwa chini ya miaka 18 na kuhesabiwa kama vijana.

Mawakili wa Bernard walisema kwamba anapaswa kupewa kifungo cha maisha gerezani bila msamaha, kwani, kwa muda wote wa gerezani, amehifadhi rekodi nzuri na alifanya kazi na mipango ya kuwafikia watu ili wasijihusishe na uhalifu.

Brandon Bernard

Nani alimtetea?

Mwendesha mashtaka wa ambaye alipinga hukumu ya kifo ya Bernard alikuwa ametaka Bernard atumikie kifungo gerezani.

Katika kipengee cha maoni kilichochapishwa katika jarida la Indianapolis Star, Angela Moore aliandika: “Baada ya kujifunza mengi tangu mwaka 2000 kuhusu kukomaa kwa ubongo wa mwanadamu na kuona Brandon akiwa mtu mzima mnyenyekevu, mwenye majuto anayeweza kuishi kwa amani gerezani, tunawezaje kusema ni miongoni mwa kundi dogo la wahalifu ambao lazima wauawe? “

Mawakili watano kati ya wanasheria tisa walitaka Bwana Trump abadilishe hukumu ya kifo ya Bernard.

Maelfu ya watu wengine walimsihi rais ampe rehema Bernard, pamoja na maseneta Richard J Durbin na Cory Brooker.

Siku ya Alhamisi, mawakili wanaoongoza Allen Dershowitz na Ken Starr pia walijiunga na timu yake ya utetezi.

Nyota wa runinga Kim Kardashian West alituma ujumbe kadhaa katika mtandao wa twitter kuhusu kesi ya Bernard kwa wafuasi wake wakati wa kuelekea kunyongwa, akiwataka wajiunge kupinga hukumu hiyo.

Kardashian West anasomea kuwa wakili huko California na hapo awali amesaidia utetezi katika kesi za uhalifu.

Mwezi Machi alitembelea Ikulu akiwa na wanawake watatu ambao hukumu yao ya kifungo cha gerezani ilikatishwa na Rais Trump.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *