img

Amshtaki mpenzi wake kwa kumpotezea muda kwa miaka 8

December 11, 2020

Mwanamke mmoja nchini Zambia amemshtaki mpenzi wake kwa kumpotezea muda na kushindwa kumuoa baada ya kuchumbiana kwa miaka nane.

Gertrude Ngoma(26) ameiambia mahakama moja nchini Zambia kuwa amechoshwa na kumsubiri mchumba wake, Herbert Salaliki(28) kumuoa baada ya kumuahidi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Getrude alikuwa bado anaishi na wazazi wake licha ya kuzaa mtoto pamoja na Herbert ambaye alikuwa anaishi pekee yake.

Herbert anaripotiwa kulipa mahari lakini bado hajamuoa mama wa mtoto wake.

Getrude amesema kuwa amechoshwa na kusubiri hivyo aliamua kumshtaki mpenzi wake kwa kutotilia maanani maisha yao ya baadaye.

“Hajawahi kutilia maanani, hii ndio sababu nilimleta kortini, Nahitaji kujua msimamo wake na hatma yetu,” amesema.

Dada huyo ameongeza kuwa ana shaka na uaminifu wa Hebert baada ya kutambua alikuwa katika uhusiano na mwanamke mwingine.

Katika kujitetea kwake, Hebert amesema hana pesa za kutosha kugharamia harusi na pia kumunyooshea kidole cha lawama Getrude kwa kutotenga muda naye.

Jaji aliyesikiliza kesi hiyo amewashauri kusameheana kama njia bora kwani bado hakuna dalili ya ndoa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *