img

Aliyeivuruga Simba kutua Yanga

December 11, 2020

KAULI aliyoitoa kiungo wa Plateau United ya Nigeria, Isah Ndala akisema amekubali kutua Yanga endapo klabu hiyo itafuata taratibu zote za kumsajili katika dirisha hili dogo la usajili, inaweza kuleta matumaini makubwa kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.

Kiungo huyo ameongeza kwamba, tayari ameshafanya mazungumzo na Yanga, anachosubiri ni kukamilisha mambo kadhaa kabla ya kuanza kuitumikia timu hiyo.

Ndala alionekana kuwavutia mashabiki wengi wa soka hapa nchini mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba uliofanyika wikiendi iliyopita Uwanja wa Mkapa jijini Dar na kumalizika kwa suluhu.

Kiungo huyo aliwavuruga vilivyo viungo wa Simba wakiongozwa na Jonas Mkude na kuonekana kulitawala eneo hilo ingawa hakuisaidia timu yake kusonga mbele.

Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka Nigeria, Ndala alisema: “Nimefanya mazungumzo na Yanga ambao wameonyesha nia ya kunihitaji kunisajili, mimi nipo tayari kujiunga na Yanga iwapo watafuata taratibu zote za usajili kwani mpira ni sehemu ya maisha yangu na kama wataleta dili zuri basi nitafanya nao kazi.“

Kuhusu mkataba wangu na Plateau huu ni msimu wangu wa mwisho, hivyo wakati uliobaki naruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote ile juu ya usajili wangu.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *