img

Wakili wa Halima Mdee aomba jalada baada ya Kibatala kujitoa

December 10, 2020

 Emmanuel Ukashu, wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Halima Mdee ameiomba  mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumpa muda wa kulipitia jalada la kesi hiyo kwa maelezo kuwa Peter Kibatala ambaye alikuwa wakili wa mteja wake amejitoa.

 Mdee anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha zisizofaa dhidi ya Rais John Magufuli.

Hayo yamejiri mahakamani hapo leo Alhamisi Desemba 10, 2020 baada ya wakili wa Serikali, Grace Mwanga kuieleza mahakama hiyo kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya utetezi na Ukashu kuomba mahakama impe muda kulipitia jalada hilo na akimaliza Mdee ataanza kujitetea.

“Wakili Kibatara ameandika barua ya kujiondoka katika kesi hii hivyo mimi ndiyo siku yangu ya kwanza nachukua hii kesi naiomba mahakama hii inipatie jalada na kuahirisha kesi hadi tarehe ijayo ili mteja wangu aanze kujitetea,” amesema Ukashu.

Baada ya maelezo hayo hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba alikubaliana na ombi hilo na shauri hilo kuahirishwa hadi Januari 19, 2021.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha kiongozi mkuu huyo wa nchi na kusababisha uvunjifu wa amani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *