img

Uturuki huenda itakwepa kiunzi cha vikwazo vya Umoja wa Ulaya

December 10, 2020

Utruki haitakumbwa na vikwazo vikali katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya, pamoja na kutolewa miito mikali kutoka kwa mataifa wanachama kama Ugiriki na Cyprus. 

Rasimu ya taarifa ya pamoja kutoka kwa viongozi wa mataifa 27 ya umoja huo, ambayo nakala yake imeonwa na shirika la habari la Ujerumani DPA, kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi hao inaonesha ishara hizo. 

Hata hivyo, kutakuwa na majina mapya ambayo yataongezwa katika orodha ya vikwazo ambayo yanazilenga kampuni zinazopigania uchimbaji wa mafuta katika mashariki mwa Bahari ya Mediterania.

 Akiwa njiani kuelekea mkutanoni, mkuu wa mashauri ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell amesema tabia ya Uturuki, bado haijawa bora tangu kufanyika mazungumzo ya mwisho ya viongozi wa Umoja wa Ulaya na kwamba mambo yamezidi kuwa mabaya.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *