img

Ujumbe wa Maalim Seif kwa wenye imani potofu

December 10, 2020

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Hamad, ameshangazwa na vijana wa chama chake ambao wapo mstari wa mbele kumkosoa na kutoa maneno badala ya kuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea maamuzi ya chama.

Akizungumza Visiwani Zanzibar katika mkutano wake na wanachama wa ACT Wazalendo amewatoa hofu huku akiahidi kusimamia  jukumu lake kutekeleza mambo yaliyoamuliwa na kikao cha kitaifa na si kama wengine wanavyodhani.

“Kuna watu wana imani potofu  wengine ni vijana wa chama chetu wanasema Maalim Seif anataka ving’ora tu , vijana wetu wanatakiwa wasimame mbele kulinda maamuzi ya chama ila wao ndio wana maneno tena cha ajabu wakati tunatoa maoni ya wananchi kabla hatujafika mbali mtu anasema Maalim Seif anataka ving’ora msidhani mimi ni limbukeni” amesema Maalim

Aidha Maalim amewataka wanachama wake kutokukata tamaa kwani ACT Wazalendo ni chama imara huku akitoa tahadhari kwa wanaodhani  huu ndio mwisho wa ACT Wazalendo

“Nawaombeni msikate tamaa, na waliyoyafanya  wasidhani wameimaliza ACT Wazalendo na hilo ndio lilikuwa lengo lao lakini aliloliweka Mwenyezi Mungu, binadamu huwezi ukaliondoa kwa uwezo wake ACT  ipo na itaendelea kuwepo na sisi hatuna kawaida ya kuvunjika moyo” amesema Maalim

Maalim Seif aliapishwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, tarehe 08/12/2020, na tangu uapisho wake kumekuwa na hali ya maneno  ndani ya chama huku mmoja wa wanachama wao akitangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *