img

Tetesi za soka kimataifa

December 10, 2020

 

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, amesema kwamba suala la kuondoka Paris St-Germain “haliko akilini mwangu”.(L’Equipe – in French)

Rais wa PSG Nasser al-Khelaifi ana “uhakika” kuwa Neymar na mshambuliaji wa Kifaransa Kyian Mbappe, 21, watakubali nyongeza ya mkataba. (L’Equipe – in French)

Chelsea ni moja kati ya klabu nne ambazo wakala wa David Alaba amezibainisha kwa ajili ya mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi, 28, ikiwa ataondoka msimu ujao. Nyingine ni Barcelona, Real Madrid na PSG.(Bild, via Sun)

Mshambuliaji wa Uholanzi Sydney van Hooijdonk,20, anaweza kuungana na klabu ya zamani ya baba yake Pierre, ya Nottingham Forest wakati mkataba wake na NAC Breda ukiwa na kipengele kinamchomruhusu kufanya uhamisho huru mwezi Januari.Mahasimu Swansea na Sheffield pia wanamtaka mchezaji huyo. (Sun)

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi atautikisa mfuko wa Paris St-Germain ikiwa mchezaji huyo wa miaka 33 atajiunga kutoka Barcelona, ​​anasema bosi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger. (Lengo)

Jordi Farre amesema kuwa ikiwa atashinda nafasi ya urais Barcelona tarehe 24 mwezi Januari, Messi atasaini mkataba mya siku inayofuata. (Sport – in Spanish)

Mshambuliaji wa Brazil Hulk, 34, yuko tayari kukatwa 90% kwa ajili ya uhamisho huru kuelekea ligi ya primia baada ya kumaliza mkataba wake na Shaghai SIPG. (Record, via Sun)

Wolves wamepewa nafasi ya kumsajili Hulk kama mbadala wa mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez aliyejeruhiwa. (Football Insider)

Bayern Munich wanajiandaa kufanya uhamisho wa kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 23. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Arsenal na Wolves ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomfuatilia mshambuliaji wa Valencia na Uruguay Mazi Gomez. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 anaweza kuuzwa mwakani. (Mail)

Wafuatiliaji kutoka Arsenal, Tottenham , Everton na Manchester United watamtazama winga wa Jamaica Leon Bailey,23, akiwa na Bayer Leverkusen ikichuana na Slavia Prague kwenye ligi ya Europa siku ya Alhamisi. (Mail)

Mshambuliaji wa Uholanzi anayekipiga PSV Eindhoven Donyell Malen, 21, yuko kwenye nafasi ya juu kwenye orodha ya Borussia Dortmund kuchukua nafasi ya Jadon Sancho,20, ikiwa watamuuza winga huyo wa Uingereza, mwakani.(Bild – in German)

Manchester United wana mashaka kama Real Madrid au Juventus wanaweza kumsajili mchezaji wao kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba,27. (ESPN)

Benfica wameamua kumpeleka kwa mkopo mchezaji wa nafasi ya ulinzi Jean-Clair Todibo,20, kurudi Barcelona mwezi Januari.(Record – in Portuguese)

Benfica pia inataka kumsajili kiungo wa kati wa Kifaransa Boubakary Soumare, 21, kutoka Lille.(A Bola – in Portuguese)

Wolves na Burnley wanamtaka mshambuliaji wa Stoke City Tyrese Campbell, lakini Stoke City tayari ilikwishaiambia Rangers kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 20 hatauzwa mwezi Januari.(Football Insider)

Toronto FC inawafanyia usaili Laurent Blanc,55, na Patrick Vieira,44, kwa ajili ya nafasi ya kocha mkuu.(Boston Globe)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *