img

Mzozo wa Tigray Ethiopia: Jinsi askari alivyonusurika makabiliano ya risassi kwa saa 11

December 10, 2020

Dakika 3 zilizopita

Ethiopian soldiers in Tigray, November 2020 - posterised effect

Askari wawili wa Ethiopia wamesimulia BBC Afaan Oromo jinsi uvamizi wa nyakati za usiku unaohusishwa na wapiganaji wa utawala wa jimbo la Tigray ulivyofanywa dhidi ya kambi yao mwezi uliyopita.

Chama cha Tigray People’s Liberation Front – ambacho kilikuwa kikidhibiti serikali ya jimbo la kaskazini- kilisema kilitekeleza shambulio kama hatua ya kujilinda wakati ulimwengu ulikuwa ukiangazia uchaguzi wa Marekani, kwani kiliamini kuwa wanakaribia kushambuliwa na vikosi vya serikali.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed alijibu mashambulio hayo kwa kuamuru oparesheni ya kijeshi ambayo kilele chake ilikuwa kupinduliwa kwa serikali ya jimbo hilo, kulazii wapiganaji wa TPLF kukimbilia milimani kupigana na kili walichotaja kuwa “wavamizi”.

Imekuwa vigumu kupata taarifa sahihi kuhusu mzozo huo kwasababu mawasiliano yalikatizwa katika jimbo hilo.

Simulizi ya askari hao zinaashiria mgawanyiko wa kikabila katika jeshi la Ethiopia, huku baadhi ya wanajeshi wa jamii ya Tigraya wakilaumiwa kwa kwa kuunga mkono TPLF.

Short presentational grey line

Nilikuwa katika kambi moja karibu na mji wa Adigrat, uliopo karibu na mpaka wa Eritrea. Mwndo wa karibu usilu saa tano unusu Novemba 3, mimi na askari wengine tulipokea ujumbe mfupi kutoka kwa askari wenzetu waliko katika kambi ya mjini Agula – karibu kilomita 30 (18 miles) kaskazini mashariki mwa mji mkuu waTigray , Mekelle – ukisema: “Tumezingirwa. Ukiweza njoo utuokoe, njoo.”

Muda mfupi baadae, kambi yetu pia ilizingirwa, na mamia ya vikosi maalum vya TPLF huku wanamgambo wakishika doria upande wa nje. Badhi ya wanajeshi wa Tigray – ambao walikuwa wameondoka kambini – walikuwa nao.

Tulimuendea kanali aliyekuwana ufunguo wa sehemu ya kuweka silaha nakumwambia afungue.

An Ethiopian solider carrying a mattress - November 2020

Maelezo ya picha,

The crisis in Tigray has revealed ethnic divisions in the Ethiopian military

Alikataa akisema hana maelekezo ya kufanya hivyo. Alikuwa kutoka jamii ya Tigray, na hapo tukashuku alikuwa sehemu ya mpango wa kutushambulia.

Baadhi ya maaskari walibishana naye kumtaka afungue sehemu ya kuhifadhi silaha; wengine walijaribu kuvunja mlango. Hatimaye, tulifanikiwakupata silaha zetu. Kufikia wakati huo wapiganaji wa TPLF tayari walikuwa wameanza kupiga risasi.

Tilichukua nafasi zetu ndani na nje ya kambi, kwa kutumia miamba ya mawe, makontena na kuta za mijengo kama kinga. Ilikuwa kama saa saba usiku mapigano yalipoanza.

Kulikuwa na umbali wa mita 50 (164ft) kati yetu na wao.

Tuliwaua zaidi ya wapiganaji 100. Na wao waliua 32 kati yetu. Katika kitengo changu, mmoja alifariki na wengine tisa kujeruhiwa.

Wanajeshi wengi waliuawa na maafisa wa Tigray waliujiunga na wapiganaji hao.

Mapigano yalidumu wa kwa saa 11 hadi saa sita mchana wakati makomanda wetu wa ngazi ya juu walipotuamuru tukomeshe mapigano, turegeshe silaha zetu stoo na kwenda katika vyumba vyetu. Tilitii amri.

Muda mfupi baadaye wachungaji na wazee kutoka mji huo walikuja. Waliomba tujisalimishe. Karibu saa kumi jioni, tuliamrishwa kupeana silaha na vifaa vyetu vya kibinasi kwa vikosi vya TPLF. Kwa mara nyingine tena, tulitii amri.

Kisha tukaambiwa tukaambiwa tuchukuwe vitu vyetu na kuingia kwenye malori. Walizunguka pamoja nasi. Tulilazimishwa kuwacha nyuma maiti.

Vikosi vya TPLF vilitusafirisha hadi kambi yao iliyopo mjini Abiy Addi, kilo mita 150 kusini magharibi mwa Adigrat.

Map
1px transparent line

Askari waliyojeruhiwa hawakupata huduma za matibabu wakati huo wote.

Kila asubuhi walitaka tujitambulishe. Ilibidi tupeane majina yetu, kabila letu na jukumu letu katika jeshi. Nilikuwa nikitoa jina la uwongo.

Sehemu hiyo nadhani ilikuwa jangwani kwasababu kulikuwa na joto sana. Tulikuwa na maji kidogo ya kunywa. Kila asubuhi tulipewa chai bila sukari katika chupa za plastiki ambazo zimekatwa nusu. Chakula chetu cha mchana kilikuwa mkate.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *