img

Mzozo wa siasa DRC: Wabunge kuamua kuhusu kumuondoa madarakani Spika wa bunge leo

December 10, 2020

Dakika 7 zilizopita

Spika Jeanine Mabunda anatoka chama cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila

Maelezo ya picha,

Spika Jeanine Mabunda anatoka chama cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila

Zaidi ya wanabunge mia mbili kati ya wabunge mia tano wameanza kikoa cha kupiga kura ya walitaka kumuondoa madarakani Spika wa bunge Jeanine Mabunda kutoka chama cha Joseph kabila.

Wabunge wa uapnde wa rais aliyeko madarakani Felix Tschisekedi wanamtuhumu kwa uongozi mbaya.

Kwa mujibu wa mbunge Moindo Nzangu , ambaye aliwasilisha mapendekezo ya kura hiyo mwanzilishi Spika Bi Jeanine Mabunda atatakiwa kujitetea mbele ya wabunge kabla ya kumpigia kura ya kutokuwa na Imani naye.

Bunge

Maelezo ya picha,

Wabunge wanamtuhumu Spika kwa kwa utendaji mbaya

Kikoa hicho ambacho kilipangwa kuanza saa nne asubuhi kimechelewa kutokana na msako na ulinzi mkali uliofanywa na vikosi vya usalama ndani ya bunge.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais Félix tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge ili apate wingi wa wabunge ambalo kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya wabunge kutoka chama cha mtangulizi wake rais mstaafu Joseph Kabila.

Félix Tshisekedi
Maelezo ya picha,

Mzozo wa kisiasa uliibuka baada ya Félix Tshisekedi kutangaza mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Jumapili Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, alitangaza kuweka mpango wa kuvunja serikali ya muungano na wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila.

Alisema alipata ushauri wa wiki tatu kabla ya kutoa tangazo hilo la kusitisha serikali ya muungano.

Bwana Tshisekedi anasema ameshindwa kutekeleza matakwa ya Wakongo kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na changamoto hiyo.

Rais mstaafu Joseph Kabila bado ana ushawishi mkubwa ndani ya siasa za DRC

Maelezo ya picha,

Rais mstaafu Joseph Kabila bado ana ushawishi mkubwa ndani ya siasa za DRC

Jambo muhimu ambalo ameliamua Rais Tschisekedi ni kuchagua maofisa wapya kuunda baraza jipya kwani bunge la sasa lina wafuasi wengi wa Kabila ambao hawamsikilizi.

Alisema alikuwa amejiandaa kuvunja bunge lote kama kuna ulazima.

“Ni wakati muafaka wa kuzingatia maadili, kanuni na mfumo wa mipango iliyopo.

Hivyo ni muhimu kufanya mageuzi yakinifu na sahihi katika bunge lililopo sasa ni muhimu”, alisema Bw Tschisekedi..

Alimteua ‘mtoa taarifa’ ,kwa mujibu wa katiba kifungu namba 78, aya ya pili.

Mtoa taarifa huyo atawajibika kuainisha watu watakaokuepo kwenye serikali mpya ya muungano, ambayo itakuwa na wajumbe wengi ambao ni wafuasi wa chama kilichopo madarakani tofauti na awali.

Kabila na Tschisekedi

Maelezo ya picha,

Huenda isiwe rahisi kwa Tschisekedi kufanya mageuzi ya kisiasa kutokana na ushawishi wa kisiasa wa mtangulizi wake Joseph Kabila

Utakuwa muungano mpya ambao serikali utauweka na kufanya kazi kwa miaka iliyosalia ya uongozi wangu, alisema alisema na kuongeza kuwa :”Kwa mujibu wa maono yangu, ili kufanikisha kukidhi matakwa ya watu mabadiliko hayo yanapaswa kufanyika.Kwa maana nyingine , sababu ya kusitisha muungano huu ni kukabiliana na mvutano uliopo ambao unaweka kizuizi katika jitihada za serikali.”

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Congo wanasema, huenda isiwe rahisi kwa Bwana Tschisekedi kufanya mageuzi ya kiuongozi ikizingatiwa kuwa kuwepo kwake madarakani kuna mkono wa mtangulizi wake Joseph Kabila ambaye bado ana ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *