img

Maseneta wa Marekani wataka Ethiopia iwekewe vikwazo

December 10, 2020

 

Maseneta wawili wa Marekani wameitolewa wito serikali yao kuzingatia kuwawekea vikwazo wanasiasa au maafisa wa jeshi watakaobainika kuhusika na ukiukaji wa haki za binaadamu katika kipindi cha mwezi mmoja cha mgogogoro wa jimbo la Tigray. 

Pendekezo hilo lilitolewa jana na Seneta Ben Cardin wa chama cha Democratic, na Seneta Jim Risch wa Republican. 

Huu unatajwa kuwa ni wito wa kwanza kabisa kutoka kwa wabunge wa Marekani, tangu kuzuka kwa mapigano Novemba 4 kati ya jeshi la serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF katika jimbo la Tigray. 

Mgogoro huo umesababisha maelfu kupoteza maisha na wengine 950,000 kuachwa bila ya makazi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *