img

Kasisi maarufu wa kanisa katoliki Nigeria awatukana waandishi wa BBC

December 10, 2020

Dakika 8 zilizopita

Kasisi Mbaka

Kasisi maarufu wa Nigeria Ejike Mbaka na baadhi ya waumini wa kanisa lake wamewatukana na kuwashambulia waandishi wa BBC na watu wengine wawili katika jimbo la kusini mashariki la Enugu Jumatano jioni.

Waandishi wa BBC Chioma Obianinwa na Nnamdi Agbanelo, pamoja na dereva wao, Ndubuisi Nwafor, walikuwa wameandamana kasisi mwingine wa kanisa katoliki, Father Cajethan Obiekezie na naibu wake Solomon Orakam, kwenda katika kanisa la padri Mbaka jumatano asubuhi.

Kasisi Obiekezie alikuwa amepanga mahojiano na Padre Mbaka, lakini mahojiano hayo hayakufanyika kwasababu alikuwa akiongoza ibada.

Waandishi wa BBC wakiongozwa na Padre Obiekezie, walienda nyumbani kwa kasisi Mbaka kufanya mahojiano karibu saa kumi na moja jioni.

FATHER MBAKA

Kasisi Mbaka alipofika nyumbani, waandishi wa BBC waliokuwa wakimsubiri ndani ya gari walipoenda kuongea naye, ghafla walizingirwa na wanaume 20.

Kwa mujibu wa Obianinwa wa BBC, wanaume hao walikuwa wamejihami kwa mapanga na walikuwa wanatishia kuwaua kwa kuandika “taarifa mbaya kumhusu Mbaka”.

“Mbaka alituomba tusubiri hadi mwisho wa shughuli za kanisa ili tufanye mahojiano. Wanaume hao waliokuwa nje ya nyumba yake walisema BBC Idhaa ya Igbo wanaandika taarifa mbaya kumhusu Mbaka na kuanza kuwapiga Nnamdi, Solomon na Ndubuisi. Waliwashambulia kwa makonde mazito mwili mzima”,Obianinwa alisema.

Mwandishi huyo wa BBC aidha alisema kasisi Mbaka na kasisi Obiekezie walitoka ndani ya nyumba waliposikia kelele na kisha kasisi Mbaka akaanza kumkaripia na kumnyoshea kidole akiimwita”shatani”.

“Hatua hiyo iliwachochea wanaume hao kuendelea kuwashambulia huku kasisi Mbaka akiendelea kupiga kelele na kututukana. Aliwaambia wanaume hao kuchukua simu na kamera zetu. Walisema watatuua na hakuna kitu kitafanyika. Walinivua wigi langu na kujaribu kumyonga Nnamdi. Kasisi Obiekezie alikuwa akiwaambia waache kutushambulia lakini yeye pia hakusazwa walimpigwa na kumpokonya simu,” alisema.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *