img

Hawa hapa wasanii watano kutoka Tanzania wanaowania tuzo za MTV Mama Awards

December 10, 2020

 

Watoto watano wa ‘JPM’ wamechaguliwa kuwania Tuzo za MTV Mama Awards ambazo zitatolewa Kampala Uganda mwanzoni mwa mwaka 2021.

ROSTAM ambao ni Stamina Roma_zimbabwe wanawania Tuzo ya Kundi Bora Afrika wakiishindani hiyo Tuzo na Sauti Sol, Ethic, Calema, Kabza de small na Dj Maphorisa, pia Blaq Diamond.

Zuchu  anawania Tuzo ya Breakthrough Act akiwa na Tems, Sha Sha, Omah Lay, John Blaq, Focalistic na Elaine.

Harmonize  anawania Tuzo ya Msanii Bora wa kiume akiipambania na Burna Boy, Fireboy DML, Innoss’B, Kabza de Small, Master KG na Rema.

Simba Diamond Platnumz anaiwania Tuzo ya Msanii bora wa mwaka kwenye kipengele kimoja na Burna Boy, Calema, Davido, Master KG, Tiwa Savage na Wizkid

Hongera sana kwa Wakali wetu wote kwa kuchaguliwa kwenye hizi Tuzo kubwa za Afrika, All the best kuipeperusha 🇹🇿!!

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *