img

Haaland atibiwa Qatar licha ya corona

December 10, 2020

Haaland, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amefunga mabao 33 katika mechi 32 kwa klabu hiyo, hatacheza mpaka Januari kutokana na kuchakina msuli wa nyonga yake na anatibiwa Qatar.

“Alitaka kwenda kwa matibabu huko,” alieleza mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc. “Amezungukwa na wataalamu ambao wana mawasiliano ya karibu sana na idara yetu ya matibabu. Ndiyo maana tulikubali ombi hilo.”

Ujerumani iliamuru duru mpya ya sheria na utaratibu wa kufunga shughuli za kila siku mwezi Novemba na kasi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona imekuwa kwa wastani 20,000 kwa wiki kadhaa.

Zorc amehalalisha kumpa ruhusa Halaand akisema wanamtarajia “azingatie sheria za usafi na arejee hapa kabla Krismasi”.

Dortmund wamefuzu kwa duru ya pili ya timu 16 bora ya mashindano ya kombe la mabingwa barani Ulaya kama vinara wa kundi lao la F na wanashika nafasi ya nne katika ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga kabla kukwaana na Stuttgart Jumamosi katika mechi ya mzunguko wa 11.

(afp)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *