img

Erdogan aizuru Azerbaijan kusherehekea ushindi wa Karabakh

December 10, 2020

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki yupo nchini Azerbaijan leo hii kwa lengo la kuungana na taifa hilo katika sherehe za kile wanachokiita ushindi wa kihistoria wa kijeshi dhidi ya Armenia, katika kuwania udhibiti wa eneo lenye mzozo la Nagorno-Karabakh.Awali taarifa ya ofisi ya Erdogan ilisema kiongozi huyo kuwasili nchini humo ni fursa ya kusherehekea pamoja kile ilichokiita “ushindi mtukufu.”

Lakini pia Erdogan amepangiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev na kisha kuongoza gwaride la kijeshi ambalo litakuwa kilele cha sherehe hizo za kitaifa za ushindi.

 Uturuki iliisadia Azerbaijan katika mapigano hayo ya majuma sita yaliyozuka mwishoni mwa Septemba, ambayo yalisababisha watu 5,000 kupoteza maisha.

 Kwa kiwango kikubwa katika mapigano hayo srikali ya Uturuki, imeshutumiwa kwa kupeleka wapiganaji mamluki kutoka Syria ili kuliimarisha jeshi la Azerbaijan, tuhuma ambazo ilizikanusha mara kwa mara.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *