img

Belle 9 afunguka mjengo aliopewa na Ridhiwani

December 10, 2020

Mkali wa muziki wa RnB Bongo Belle 9 ameshea stori ya kupewa mjengo kutoka kwa mtoto wa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Belle 9 amesema amepewa mjengo huo uliopo fukwe za Mikocheni kwa ajili ya uzinduzi wa video ya wimbo wake wa ‘give it to me’ pia anamshukuru Ridhiwani Kikwete kwani hakuwahi kupata sapoti yoyote kutoka kwa wanasiasa zaidi yake.

“Namshukuru sana Mh Ridhiwani Kikwete kwa sababu sijawahi kupata sapoti yoyote kutoka kwa mwanasiasa wa chama chochote kunifanyia kitu kikubwa kama kile kiukweli Mungu ambariki sana, aliweza kunipa ‘beach house’ yake ya Mikocheni kufanya uzinduzi wa video yangu, ilikuwa kama zawadi na kitu kikubwa kwangu sitaweza kusahau” ameeleza Belle 9 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *