img

Alichokisema Jaji Warioba kuhusu Haki za binadamu

December 10, 2020

 

Katika Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kituo Cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeadhimisha siku hii leo kwa kuhamasisha amani huku kauli mbiu ikiwa ni “Haki ni Maendeleo, Simamia Haki”.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na taasisi mbalimbali za kupinga ukatili, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, amesema kuwa vurugu huingilia haki za binadamu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa LHRC,Anna Henga amewataka wanajamii kuacha kukaa kimya pindi vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unatokea.

Aidha, wamewataka wananchi wote kuilinda amani ya nchi kwani amani isipoimarika kutatokea vurugu na kushindwa kulinda haki za binadamu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *