img

December 10, 2020

 

Waziri wa Maji nchini Tanzania,  Jumaa Aweso amemsimamisha kazi mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (Duwasa), David Palangyo kumtaka asubiri kupangiwa kazi nyingine.

 Akizungumza leo Alhamisi Desemba 10, 2020 Aweso ambaye ameapishwa jana na Rais John Magufuli amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa Palangyo kwa maelezo kuwa Jiji la Dodoma linahitaji mtendaji mwenye kasi zaidi.

Amesema kuondolewa kwa kiongozi huyo iwe ishara kuwa hatakuwa tayari kufanya kazi na watu wazembe na ambao hawaendi na kasi ya Rais Magufuli.

“Najua kaka yangu umefanya kazi kubwa, hata hivyo lazima tuwe wa kweli kwamba Dodoma tunahitaji kasi zaidi kwa kuwa macho ya viongozi yanatazama hapa, sitakuwa mpole naomba utupishe utapangiwa majukumu mengine baadaye,” amesema Aweso.

Kiongozi huyo amesema hawezi kudanganywa kwa namna yoyote kwa kuwa anaifahamu Duwasa kuliko wanavyodhani na jicho lake liko hapo.

Amesema ni wakati wa watumishi wazembe kukaa mguu sawa na ikibidi waanze kupisha wenyewe na kusisitiza a kuwa atawapa ushirikiano mkubwa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini ambao watakuwa wakiwajibika.

Waziri Aweso amewaonya watumishi wa Duwasa watakaoanza kukwamisha kazi ya mkurugenzi atakayeteuliwa, “hao ndio watakuwa wa kwanza kuondoka kabla ya huyo aliyepewa jukumu hilo.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *