img

Wananchi watakiwa kutoa mashirikiano katika kutunza miundombinu

December 9, 2020

NA THABIT MADAI,ZANZIBAR.

WANANCHI wametakiwa kuwa na mashirikiano katika kutunza miundombinu inayoanzishwa na Serekali ili kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu kwa lengo la  kuwaletetea maendeleo na kurahisisha shughuli zao za kutafuta kipato.

Akizungumza wakati wa uchimbaji wa misingi na kutandaza mipira ya maji katika shehia ya ubago katika jimbo la Tunguu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali (Kichupa) amesema utunzaji wa miundombinu ni suala muhimu nchini kwa hupunguza gharama za serikali katika kukarabati miundombinu mara kwa mara.

Amesema Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar kwa kuwaondoshea changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo huduma ya  maji , umeme na barabara ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Uchumi wa Buluu.

Aidha amesema maendeleo hayo yatafikiwa kwa mashirikiano wa viongozi wa Jimbo, Wananchi pamoja na Serikali ili kuzitatua changamoto zinazowakabili wananchi.

 Nae Mbunge wa Jimbo la Tunguu Khalifa Salum Suleiman amesema ilani ya Chama Cha Mapinduzi inawataka viongozi wa Jimbo kuwa watatuzi na wasimamizi wa miradi ya Maendeleo inayoanzishwa na Serekali ili kuhakisha inawafikia walengwa waliokusudiwa.

Ameeleza kuwa wakati wa kuwaomba kura wananchi walitoa ahadi ya kuwaondolea kero zilizopo kwenye maeneo yao na sasa wana wajibu baada ya kushinda wa kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizotoa.

‘’Tulipokuja kuwaomba kura tuliwaahidi kuwa tutayatatua matatizo, hivi sasa wakati umefika wa kutekeleza kwa vitendo yale tuliyoahidi’’ alisema Mbunge huyo

Wakati huo huo diwani wa Wadi ya Ubago Ussi Ali Mtumwa amewataka wananchi wa kijiji cha Mwera Pongwe kuzitunza na kuzitumia vizuri huduma zinazotolewa na Serekali kwa kushirikiana na jimbo kwani zinatumia gharama kubwa kuwafikia wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Bi Paulina Msalaba amesema wananchi wa kijiji hicho wanampongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kuwaletea huduma ya maji kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma hiyo muhimu kwa binadamu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *