img

Virusi vya corona Mashariki na Afrika

December 9, 2020

 

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona (Covid-19) kote ulimwenguni  imezidi 1,565,800. Idadi ya kesi za maambukizi imezidi 68,691,000, na idadi ya wagonjwa waliopona imezidi 47,591,000.

Katika nchi ya India, idadi ya watu waliofariki kwa covid-19 imepanda hadi kufikia 141,398. Idadi ya kesi za maambukizi ya corona nchini humo nayo imefikia 9,735,000.

Iran pia imeripoti vifo 51,212 vya corona na kesi 1,072,000 za maambukizi ya virusi hivyo.

Katika nchi ya Urusi, idadi ya vifo vinavyotokana na janga la covid-19 imeripotiwa kuwa  44,718. Idadi ya kesi za maambukizi nayo imefikia 2, 541,000 nchini humo.

Katika nchi ya Korea Kusini ambapo watu 556 wamefariki kwa corona, Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa kimetangaza kugundulika kwa kesi 686 mpya za maambukizi ya covid-19 ndani ya masaa 24 na idadi yote kufikia 39,432.

Nchi ya China ambayo ndio chimbuko la covid-19, idadi ya vifo imeripotiwa kuwa 4,634 hadi kufikia sasa. Kulingana na taarifa iliyotolewa na Tume ya Kitaifa ya Afya ya China, iliarifiwa kugundulika kwa kesi 11 mpya za maambukizi za ndani ya nchi kwa masaa 24 na kesi nyingine 15 mpya za maambukizi za nje ya nchi zilizopelekea idadi yote ya maambukizi kufikia 86,661.  Haikuripoti idadi yoyote ya vifo ndani ya masaa 24 ya mwisho.

Kulingana na taarifa za Wizara ya Afya nchini Tunisia, hadi kufikia leo watu 3,596 wamepoteza maisha kwa covid-19 nchini humo. Idadi ya kesi za maambukizi imeripotiwa kufikia 104,329. Wahudumu wa afya wameandaa maandamano kwa ajili ya kupinga taratibu za kazi.

Katika nchi ya Israel ambapo kumeripotiwa vifo 2,932 na kesi 348,968 za maambukizi, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, alitoa maelezo baada ya kuwailisha chanjo 100,000 za Covid-19 za Pfizer na kusema kuwa chanjo hizo zitatolewa kwa raia wa Israel kwanza. Aliongezea kusema,”Tunaiamini chanjo ya Pfizer na nitakuwa mtu wa kwanza kufanyiwa chanjo ili niwe mfano kwa wananchi wa Israel.”

Na katika bara la Afrika, idadi ya vifo vinavyotokana na covid-19 kwa ujumla imeripotiwa kufikia 54,611 baada ya kuongozeka kwa vifo 402.  Idadi ya kesi za maambukizi nayo imeripotiwa kufikia 2,300,810 baada ya kuongezeka kwa kesi 13,046 ndani ya masaa 24. . Idadi kubwa ya vifo imeripotiwa Afrika Kusini ambayo imepita 22,432. Nchi ya Misri inafuata kwa idadi ya vifo 6,813 na Morocco kwa idadi ya vifo 6,370.

Katika nchi ya Indonesia, idadi ya vifo imepanda hadi kufikia 18,171 na idadi ya kesi za maambukizi imefikia 592,900.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *