img

Tamasha la mitido kufanyika Disemba 19 mwaka huu

December 9, 2020


Na Thabit Madai,Zanzibr.

TAMASHA kubwa la mitindo visiwani Zanzibar linalojukana kwa jina la ‘RUN WAY BAY’ linatarajiwa kufanyika Disemba 19, 2020 huku Wajasiramali pamoja na wabunifu nchini wametakiwa kujitokeza kushirki katika tamasha hilo kwa lengo la kuonesha na kuuza bidhaa zao.

Tamasha hilo linatarajwa kufanyika siku Tatu (3) na kuwajuisha wajasiriamali na wabunifu wa kazi za Sanaa tofauti tofauti kutoka Zanzibar nan je ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maru maru mzingani mjini Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Waiz Houston Shezukindo amesema kwamba  ni vyema wajasiriamali na wabunifu wa kazi mbalimbali za Sanaa  kuitumia fursa hiyo kwa  kutangaza bidha zao wanaozalsha.

Alisema Tamasha hilo ni njia moja wapo kwa wajsiriamal na wabunifu nchini kujongozea kipato cha kila siku na kujikamua na maisha.

“Kupita Tamasha hili, wajasiriamali na wabunifu wa kazi  mbalimbali za sanaa watapata kujitagaza na kujihakikishia wanasoko la kudumu na kujiogezea kipato chao cha kila siku,” amesema Shezukindo.

Aidha, alisema tamasha hilo kutakuwa kwa muda wa siku tatu ambalo litahusisha mitindo mbali mbali ikiwemo mavazi na limelenga kutengeneza ajira kwa vijana na kuwapatia fursa ya kuibua vipaji vyao.

Alieleza, kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwazindua vijana ambao hawana ajira ambapo kupitia tamasha ilo vijana watapata kujiajiri kupitia sekta ya mitindo na kukamilisha ndoto zao.

Alifafanua kuwa tamasha litazingatia  maadili ya kizanzibar na kufuata taratibu na utamaduni wa Zanzibar kwa kupitia mila, silka na desturi.

“Tumeona umuhimu  wa kuibua vipaji na kuwapati fursa wajasiriamali kuuza biashara zao pamoja na wasanii kuonyesha vipaji vyao na kupata kujitangaza ndipo tukaandaa tamasha hilo”alisema 

Kwa upande wake mwanamitindo Shekha Muhsin Othman, aliwasisitiza vijana kujiajiri wenyewe na kuacha kusubiri ajira kutoka serikalini  ili kukidhi mahitaji yao na kukuza pato la taifa.

“Vijana amkeni msilale musitegemee kuajiriwa na serikali tumieni fursa za kujiajiri wenyewe “alisema.

Tamasha hilo limeadaliwa  na Waiz Houston Shezukindo  ambao hufanyika takribani kila mwaka ambapo kwa mwaka huu limekuja na kauli mbiu isemayo ‘Ndoto yangu kipaji changu,Maisha yangu’.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *