img

Ni kwanini mwanamfalme wa Saudi Arabia Muhammed bin Salman hatayawezi masharti haya?

December 9, 2020

Dakika 5 zilizopita

A handout photo shows Saudi Arabia's Crown Prince Mohammed bin Salman at the G20 Riyadh Summit, Riyadh, Saudi Arabia (21 November 2020)

Hizi ni siku ambazo sio nzuri kwa uongozi wa Saudi Arabiahusasan kwa mwanamfalme mwenye mamlaka makubwa Mohammed bin Salman, al maarufu MBS.

Nyumbani bado ni maarufu, lakini kimataifa hajaweza kuondokana na jinamizi la kushukiwa kwa madai ya uhusika wake katika mauaji ya kikatili ya mwaka 2018 dhidi ya mwandishi wa habari wa Saudia Jamal Khashoggi.

Na sasa utawala mpya wa Marekani unajiandaa kuhamia katika Ikulu ya White House na Rais mteule Joe Biden amekwishatangaza wazi kwamba atachukua msimamo wa hatua kali zaidi ya mtangulizi wake katika masuala fulani ya misimamo ya Saudi Arabia

Je ni masuala gani anayoyazungumzia na ni kwanini ni muhimu kwa wale waliopo madarakani Washigton na Riyadh?

2px presentational grey line

Vita hivi vimekuwa ni maafa kwa takriban kila mtu aliyehusika, lakini zaidi kwa Wayemen masikini na idadi ya watu wenye utapiamlo nchini humo.

Saudi Arabia haikuanzisha mzozo huu- Wahudhi walianzisha vita hivi wakati walipoingia katika mji mkuu Sanaa mwishoni mwa mwaka 2014 na kuing’oa madarakani serikali halali. Wahuthi ni kikundi cha kikabila kutoka eneo la milima la kaskazini mwa nchi , wakiwa ni sawa na 15% ya idadi ya watu wa Yemen.

Mzozo wa Yemen umesababisha njaa na utapiamlo miongoni mwa raia wa nchi hiyo wakiwemo watoto
Maelezo ya picha,

Mzozo wa Yemen umesababisha njaa na utapiamlo miongoni mwa raia wa nchi hiyo wakiwemo watoto

Mwaka 2015, Mohammed bin Salman, akiwa waziri wa ulinzi wa Saudia , kwa siri aliyaunganisha mataifa ya kiarabu halafu wakaingia vita kwa mashambulio makali ya anga, wakitarajia kuvilazimisha vikosi vya Wahudhi kusalimu amri ndani ya miezi michache.

Baada ya miaka takriban sita, huku maelfu wakiuawa na wengine kusambaratika, na uhalifu wa kivita kutrekelezwa na pande zote, muungano ulioongozwa na Saudi Arabia umeshindwa kuwaondoa Wahuthi katika mji mkuu Sanaa na katika maeneo ya magharibi mwa Yemen.

Kwa usaidizi kutoka Iran, Wahuthi , wamekuwa wakifyatua makombora ya masafa yaliyosababisha maafa na vilipuzi kwa kutumia droni ndani ya Saudi Arabia, na kupiga mitambo ya mafuta hadi katika maeneo ya mbali kama Jeddah.

A boy rides with Houthi supporters in a vehicle during a funeral in Sanaa, Yemen (22 September 2020)

Maelezo ya picha,

Muungano unaoongozwa na Saudia umeshindwa kuwaondoa Wahuthi katika mji wa Sanaa

Ni vita vyenye garama visivyoisha na mipango mbalimbali ya amani imevunjika, mmoja baada ya mwingine.

Vita vya Yemen vinawauwa Wayemen na kuharibu mali za Saudia, huku vikikosolewa vikali nje ya nchi.

Wasaudia wangependa kupata njia ya kuondoka katika vita hivyo. Lakini kama walivyosema kwa maneno yao wanataka , ” kuizuia Iran kukanyaga katika mpaka wao wa kusini “, wanasisitiza kuwa hawawezi kukubali wanamgambo wenye silaha wanaoungwa mkono na Iran kushikilia mamlaka nchini Yemen.

Debris seen in front of Saudi Aramco oil facility in Jeddah that the Houthis said they attacked (24 November 2020)

Maelezo ya picha,

Wahudhi walisema walifanya shambulio la kombora la masafa marefu dhidi ya kituo cha mafuta kilichopo Jeddah mwezi uliopita.

Hata hivyo muda unakwisha wa vjuhudi za vita kwa upande wa Saudia

Mwaka 2016, mwishoni mwa utawala wa rais , Barack Obama tarari Marekani ilikuwa imeanza kubana baadhi ya msaada wake kwa Saudia. Donald Trump aliondoa sera hiyo na kuipatia Riyadh msaada wote wa kiintelijensia na vifaa iliyouhitaji. Sasa utawala wa Bw Biden umekwishaashiria kuwa hilo kuenda halitawezekana.

Shinikizo linaendelea kuitaka imalize vita hivi, kwa njia moja au nyingine.

Wanawake waliofungwa

Suala hili limekuwa balaa kwa uhusiano wa kimataifa kwa utawala wa Saudia

Wanaharakati kumi na watatu wanawake wa amani wamefungwa na wakati fulani katika unyanyasaji wa kutisha, kwa kosa uhalifu wa kudai haki ya kuendesha magari na kumazilika kwa mfumo wa ubaguzi mkubwa ambao unawalazimu wanawake kutembea na walinzi wa kiume.

Mwanamke wa Saudia akiendesha gari kwa mara ya kwanza
Maelezo ya picha,

Mwanamke wa Saudia akiendesha gari kwa mara ya kwanza

Wengi wakiwemo Mwafungwa maarufu kama Loujain al-Hathloul, wakikamatwa mwaka mwaka 2018, kabla ya marufuku ya wanawake kuendesha magari kuondolewa.

Loujain al-Hathloul (file photo)

Maelezo ya picha,

Loujain al-Hathloul alikuw amtu maarufu katika kampeni ya kushinda haki ya wanawake wa Saudia kuendesha magari

2px presentational grey line

Suala hili linaonekana nje kwamba lilitatuliwa naada juhudi kubwa kufanyika nyuma ya pazia kwa upatanishi wa Kuwaiti . Hata hivyo tatizo bado ni kubwa.

Mwaka 2017, katika kipindi cha siku kadhaa cha ziara ya Rais Trump mjini Riyadh, Saudi Arabia ilijiunga na Muungano wa nchi za kiarabu, Bahrain na Misri kuwasusia majirani zao wa Ghuba Qatar.

Egyptian President Abdul Fattah al-Sisi, Saudi Arabia's King Salman and US President Donald Trump place their hands on a globe at the World Center for Countering Extremist Thought in Riyadh, Saudi Arabia, 21 May 2017

Maelezo ya picha,

Ususiaji wa Qatar ulianza muda mfupi baada ya ziara ya Donald Trump mjini Riyadh mwaka 2017

Sababu waliyosema ilikuwa ni kwasababu uungaji mkono wa Qatar usiokubalika wa makundi ya Kiislamu yanayofanya ugaidi.

Muungano wa nchi za kiarabu UAE ulitoa nyaraka za madai kuwa magaidi walikuwa wanaishi Qatar, lakini nchi hiyo ilikataa kuunga mkono ugaidi na kupinga madai ya mataifa hayo matatu kwamba isitishe matangazo ya televisheni yake ya Al Jazeera.

A picture taken on 5 December 2019 shows a general view of the headquarters of the Al Jazeera Media Network, in Doha, Qatar

Maelezo ya picha,

Wasaudia na washirika wake waliitaka Qatar ifunge televisheni yake ya Al Jazeera

Kwa upande mwingine Qatar, Uturuki na mavuguvugu mengine mabli mbali ya kisiasa ya Kiislamu wote waliunga mkono miungano kama vile Muslim Brotherhood na Hamas mjini Gaza.

Mavuguvugu haya ya kimataifa hayapendwi na viongozi wa nchi hizo tatu , ambazo zinayaona kama tisho lililopo kwa utawala wao.

Hakuna swali kwamba ususiwaji wa Qatar wa miaka takriban mitatu umeathiri pande zote kiuchumi na kisiasa.

Pia umeathiri umoja wa mataifa ya Ghuba ya kiarabu katika wakati ambapo viaongozi wa ghuba ya uarabu wakiendelea kuwa na hofu dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran na mipango yake ya makombora ya masafa marefu.

US envoy Jared Kushner (L) meets Qatar's Emir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani (R) in Doha (2 December 2020)

Maelezo ya picha,

Mshauri wa rais Trump Jared Kushner alifanya mazungumzo na Amir wa Qatar mjini Doha wiki iliyopita

Mjumbe wa Rais Trump Jared Kushner amekuwa katika Ghuba kujaribu kusaidia kumalizika kwa mzozo, na utawala wa Biden utataka kuona mzozo huu ukitatuliwa. Qatar ina ngome kubwa zaidi ya Pentagon nje ya Marekani iliyopo katika eneo la Al-Udaid.

Lakini kwa upatanishi wowote utakaokubaliwa utahitaji bado kuwa ni wa kivitendo.

Itachukua miaka kwa Qatar kuwasamehe majirani zake na itawachukua miaka kuiamini Qatar tena.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *