img

Nchi tajiri zinahodhi chanjo ya Covid, Shirika la Umoja wa chanjo ya watu imeeleza

December 9, 2020

Dakika 11 zilizopita

Chanjo

Nchi tajiri zinaweka akiba ya chanjo ya Covid huku watu wanaoishi katika nchi masikini wakikosa umoja wa mashirika ya kampeni umeonya

Umoja wa Chanjo ya Watu unasema karibu nchi 70 zenye kipato cha chini zitaweza kutoa chanjo kwa mtu mmoja kati ya watu 10.

Hii ni licha ya Oxford-AstraZeneca kuahidi kutoa asilimia 64 ya dozi zake kwa watu katika mataifa yanayoendelea.

Hatua zinachukuliwa kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa chanjo kote ulimwenguni.

Ahadi hii ya chanjo, inayojulikana kama Covax, imeweza kupata dozi milioni 700 za chanjo zitakazosambazwa kati ya nchi 92 za kipato cha chini ambazo zimejiandikisha.

Lakini hata kwa mpango huu uliopo, Umoja wa Chanjo ya Watu – mtandao wa mashirika ikiwa ni pamoja na Amnesty International, Oxfam na Global Justice Now – unasema kuwa haitoshi kuzunguka, na kampuni za dawa zinapaswa kushirikisha teknolojia yao ili kuhakikisha dozi zaidi zinatengenezwa .

Uchambuzi wao uligundua kuwa nchi tajiri zimenunua dozi za kutosha kuchanja watu wao wotemara tatu ikiwa chanjo zote zitaidhinishwa kutumiwa.

Canada, kwa mfano, imeamuru chanjo za kutosha kumtosheleza kila raia wa Canada mara tano,

Na ingawa mataifa tajiri yanawakilisha asilimia 14 tu ya idadi ya watu ulimwenguni, wamenunua 53% ya chanjo zote zilizoonesha matumaini ya kufanya kazi mpaka sasa.

“Hakuna mtu anayepaswa kuzuiwa kupata chanjo ya kuokoa maisha kwa sababu ya nchi wanayoishi au kiwango cha pesa mfukoni mwake,” alisema Anna Marriott, meneja wa sera ya afya ya Oxfam.

“Lakini isipokuwa kitu kitabadilika sana, mabilioni ya watu ulimwenguni hawatapokea chanjo salama na bora ya Covid-19 kwa miaka ijayo.”

Umoja wa Chanjo ya Watu unatoa wito kwa mashirika yote ya dawa yanayofanyia kazi chanjo za Covid-19 kushirikisha kwa uwazi teknoloji ili mabilioni ya dozi zaidi yaweze kutengenezwa na kupatikana kwa kila mtu anayezihitaji.

AstraZeneca, kampuni inayotengeneza chanjo ya Covid iliyoundwa na Chuo Kikuu cha Oxford, imesema itahakikisha kuwa inapatikana kwa njia isiyo ya faida kwa nchi zinazoendelea.

Ni ya bei rahisi kuliko nyingine na inaweza kuhifadhiwa kwenye friji, na kuifanya iwe rahisi kuisambaza kote ulimwenguni.

Lakini wanaharakati wanasema kampuni moja peke yake haiwezi kutoa chanjo za kutosha kwa ulimwengu wote.

Chanjo ya Pfizer-BioNTech tayari imepata idhini nchini Uingereza na walio hatarini zaidi wanaanza kupatiwa chanjo wiki hii. Inawezekana kupokea idhini kutoka kwa wasimamizi huko Marekani na Ulaya hivi karibuni, ikimaanisha inaweza kuwa muda kidogo kabla ya kupelekwa katika mataifa masikini.

Chanjo nyingine mbili, kutoka Moderna na Oxford-AstraZeneca, zinasubiri idhini ya kisheria katika nchi kadhaa.

Chanjo ya Urusi, Sputnik, pia imetangaza matokeo mazuri ya majaribio, na chanjo nyingine nne zinapitia hatua za mwisho za majaribio.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *