img

Mohsen Fakhrizadeh: Iran ‘yawakamata’ waliohusika katika mauaji ya mwanasayansi

December 9, 2020

Dakika 2 zilizopita

Prominent Iranian scientist Mohsen Fakhrizadeh in an undated photo

Maelezo ya picha,

Mohsen Fakhrizadeh alikuwa mkuu wa Shirika la uvumbuzi wa kiulinzi na utafiti la Iran

Baadhi ya watu waliohusiaka katika mauaji ya mwanasayansi wa ngazi ya juu wa Iran wamekamatwa , amesema mshauri wa bunge nchini humo.

Hossein Amir Abdollahian aliiambia televisheni ya Al-Alam kwamba hakuweza kushirikisha maelezo ya watu hao kwasababu za kiusalama, lakini wahusika hawatautoroka mkono wa sheria.

Amesema kuwa kuna ushahidi wa uhusika wa Israel katika mauaji hayo. israeli haijathibitisha wala kukana kuwajibika na mauaji hayo.

Mwanasayansi huyo, Mohsen Fakhrizadeh, aliuawa karibu na mji wa Tehran tarehe 27 Novemba.

Maafisa nchini Iran wametoa ushahidi unaokinzana kuhusu jinsi alivyopigwa risasi hadi kufa alipokuwa akisafiri katika msafara wa magari kupitia mji wa Absard.

Katika siku ya shambulio, wizara ya ulizi ilisema kulikuwa na mapigano baina ya walinzi wake na watu kadhaa wenye silaha . Ripoti ya Iran iliyoelezea kauli za mashahidi ilisema kuwa ” washambuliaji kati ya watatu na wanne ” waliuawa.

attack scene

Maelezo ya picha,

Bunduki ya machine-gun inayoongozwa kwa kifaa ilifyatua risasi 13 katika gari la Mohsen Fakhrizadeh , kwa mujibu wa Brigadia Jenerali Ali Fadavi

Lakini Jumapili , Kamanda jeshi la Iran la -senior Revolutionary Guardsalisema silaha iliyotumia setilaiti ya intelijensia bandia ndiyo iliyofyatua gari lake

Brigadia -Jenerali Ali Fadavi aliviambia vyombo vya habaro nchini humo kuwa silaha yenye ukubwa wa lori aina ya pick-up ,liliweza kuvuta picha ya ichwa cha mwanasanyansi huyo na kukilenga kwa risasi bila kumdhuru mke wake aliyekua kando yake.

Madai hayo hayta hivyo hayakuthibitishwa na duru huru na wataalamu wa silaha za kielectroniki walishuku maelezo hayo.

Je Fakhrizadeh alikufa vipi?

assassination scene

Maelezo ya picha,

Barabara karibu na Tehran ambako watu wenye silaha walimshambulia Mohsen Fakhrizadeh

Maelezo ya Iran kuhusu kile kilichotokea siku ya kifo chake yamekuwa yakibadilika sana lakini inaonekana kwamba Fakhrizadeh alijeruhiwa na kufa baada ya gari lake kushambuliwa kwa risasi nyingi katika mji wa Absard, mashariki mwa Tehran.

Wakati wa shambulio hilo imeripotiwa kuwa bomu katika gari la Nissan pickup pia lililipuka.

Picha katika mitandao ya kijamii zinaonesha vifusi , damu kando ya barabara, na gari lililopigwa risasi.

Waziri wa ulinzi aliripoti kuwa kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya walinzi wa Fakhrizadeh na watu kadhaa waliokuwa na silaha.

Ripoti moja ya Iran iliwanukuu walioshuhudia tukio la mauaji hayo wakisema”watu wanne wanaosemekana kuwa walikuwa ni magaidi, waliuawa.”

Vyombo vya habari vya Iran vilisema mwanasayansi huyo wa nyuklia aliuliwa na “bunduki inayoongozwa ” au silaha “zinazoongozwa na satelaiti “.

Na Jumatatu, Rear Admiral Shamkhani,anayeongoza Baraza la ngazi ya juu zaidi la usalama, alithibitisha kuwa lilikuwa shambulio lililoongozwa kwa mbali, kwa kutumia “mbinu maalum “.

Ni kwanini Fakhrizadeh alilengwa?

Israeli na vyanzo vya usalama vya magharibi wanasema kuwa alikuwa mtu muhimu sana katika mpango wa nyuklia wa Iran.

Profesa huyo wa fizikia anasemekana kuwa aliongoza mradi wa Amad “Project Amad”, mpango ambao Iran inadaiwa kuuanzisha mwaka 1989 ili kufanya utafiti wa uwezekano wa kutengeneza bomu la nyuklia.

Students wearing facemasks and holding signs saying "Down with Israel" and others in Farsi burn Israeli and US flags in Tehran at a protest outside Iran's foreign ministry in Tehran (28 November 2020)

Maelezo ya picha,

Mwaka 2018, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alifichua kile alichodai ni makavazi ya siri ya atomiki ya Iran

Presentational grey line

Mradi huo ulifungwa mwaka 2003, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la nishati ya Atomiki, ingawa Waziri Mkuu Nettanyahu alisema mwaka 2018 kwamba nyaraka ambazo nchi yake ilizipata zilionesha kuwa Fakhrizadeh aliongoza mpango ambao ulikuwa unaendelea kwa siri wa kazi ya ”Project Amad’.

Katika maelezo yake, Bw Netanyahu aliwataka watu “kulikumbuka jina hilo “.

Awali Iran iliishutumu Israel kwa mauaji ya wanasayansi wengine wanne wa nyuklia wa Iran kati ya mwaka 2010 na 2012.

Wachambuzi wanahisi kuwa mauaji ya hivi karibuni hayakulenga kuangamiza mpango wa nyuklia wa Iran bali yanalenga kumaliza matarajio ya Marekani ya kujiunga tena na mkataba wa nyuklia wa Iran wa 2015 wakati Rais mteule Joe Biden atakapochukua rasmi mamlaka mwaka ujao.

Waziri Mku wa Israel Benjamin Netanyahu alifichua mpango wa siri wa nyuklia wa Iran, ambapo alishutumu Mohsen Fakhrizadeh kuhusika
Maelezo ya picha,

Waziri Mku wa Israel Benjamin Netanyahu alifichua mpango wa siri wa nyuklia wa Iran, ambapo alishutumu Mohsen Fakhrizadeh kuhusika

Rais Donald Trump alijiondoa katika mkataba mwaka 2018, akisema ulikuwa saying “umekiuka madhumuni yake “, na kuweka tena vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran katika juhudi za kuwalazimisha viongozi wa Iran kufanya mazungumzo ya kuubadilisha.

Iran imekataa kufanya hivyo na ikajibu kwa kuvunja vipengele muhimu vya mkataba huo , kama vile kuongeza kiwango chake cha urutubishaji wa madini ya Uranium.

Urutubishaji wa uranium unaweza kutumiwa kuchochea nyuklia na pia unaweza kutumiwa kutengeneza mabomu ya nyuklia.

________________________________________

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *