img

Mjue naibu waziri aliyeshindwa kula kiapo

December 9, 2020

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema atamteua naibu waziri mwingine wa Madini baada ya aliyemteua Desemba 5, 2020, Francis Ndulane kushikwa kigugumizi wakati akila kiapo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatano Desemba 9, 2020.

Ndulane ambaye ni mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) mwenye elimu ya shahada ya uzamili ameshindwa kusoma kiapo mbele ya Rais Magufuli,akikosea mara kadhaa kila alipopewa nafasi ya kurudia kusoma na ndipo katibu mkuu kiongozi,  John Kijazi kumtaka aende kuketi kwanza.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, Ndulane ana elimu ya shahada ya uzamili katika uhasibu na fedha ambayo ameisomea katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 na 2015. Pia, ana stashahada ya juu ya uhasibu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).

Ndulani alisoma shule ya msingi Uwanjani (mwaka 1980 – 1986), baadaye akaenda sekondari ya Tambaza (mwaka 1987 – 1990) na baada ya kuhitimu kidato cha nne, alikwenda sekondari ya Pugu (mwaka 1991 – 1993).

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *